Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Dr.Suleiman Serera akikabithi pikipiki(boda boda ) sita zenye thamani ya shilingi milioni kumi na nne na laki moja ikiwa ni mkopo kwa kikundi cha vijana kiitwacho Bodaboda Familiy kilichopo katika mji mdogo wa Orkesumet Wilayani Simanjiro,Sherehe hizo zilifanyika leo tarehe 24/11/2021 katika ukumbi wa Wilaya ya Simanjiro.
Mh.Dr Suleiman Serera Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro (katikati,aliyevaa suti nyeusi) katika warsha ya kukabidhi pikipiki sita zenye thamani ya shilingi milioni kumi na nne na laki moja kwa kikundi cha Bodaboda Familiy ikiwa ni mkopo kwa kikunldi hicho cha vijana.
Pia Mh.Mkuu wa Wilaya alikabithi hundi ya Mfano ya shilingi 213,383,239.67 ikiwa ni fedha zitakazo tolewa kwa vikundi vya wanawake vijana na watu wenye ulemavu Wilayani Simanjiro zilizotokana na marejesho pamoja na mapato ya ndani ya Halmashauri.
Habari kamili:
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Simanjiro Bi.Asia Ngalisoni akisoma risala mbele ya Mgeni Rasmi (Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro(Mh.Dr.Suleiman Serera)) leo tarehe 21/11/2021 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro wakati wa sherehe za kukabithi Bodaboda sita kwa kikundi cha Bodaboda Family Kilichopo katika Kata ya Orkesument katika Wilaya ya Simanjiro.
Bi.Asia alisema kuwa katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021/2022 yaani mwenzi july hadi September 2021 Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro imetoa kiasi cha shilingi 213,383,239.67 ambazo kati ya hizo shilingi milioni sabini (70) ni asilimia kumi ya mapato ya ndani na shilingi 134,117,000 ni fedha za marejesho ya awali ,ambapo wanachama 203 walinufaika na mikopo hiyo.
Aidha alisema vigezo vya kuanzisha kikundi cha wanawake au vijana ni kama ifuatavyo:
1.mwanachama lazima awe na umri wa miaka kumi na nane na kuendelea
2.Kikundi lazima kiwe na wanachama watano na kuendelea
Aidha masharti ya kikundi cha walemavu ni kama ifuatavyo:
1.Mwanachama lazima awe na umri wa miaka kumi na nane na kuendlea
2.Kikundi lazima kiwe na wanachama wawili na kuendelea
Aidha katika kijiji au eneo moja ambapo watakosekana walemavu wawili basi mlemavu huyo mmoja taweza kupatiwa mkopo huo.
Pia alisema kwa robo ya kwanza ya mmwaka wa fedha 2021 Halmashauri imepokea kiasi cha shilingi 122,041,000 kutoka kwa vikundi ikiwa ni kwa ajili ya marejesho ya vikundi vilivyokopa awali.
Aliongeza kwa kusema kuwa idara ya Maendeleo ya Jamii ya Wilaya ya Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro inaendelea Kufuatilia fedha za marejesho kwa vikundi vilivyokopa awali ali zitumike kukopesha vikundi vyenye uhitaji pamoja na vikundi vipya vinavyoanzishwa.
MKUU WA TAKUKURU(W).
Kamanda wa Takukuru(W) ya Simanjiro.
Kamanda wa Takukuru wa Wilaya ya Simanjiro aliipongeza Halmashauri kwa jitihada zake za kuwakwamua wananchi kutoka katika umasikini na utegemezi kwa kuwakopesha fedha kwa masharti nafuu na bila riba.
Aidha aliwataka wananchi kuacha kuwatumia wanasiasa kwa kuwaomba kuwasaidia kuongea na wataalamu wa Halmashauri ili waweze kupata mikopo hiyo kiurahisi na kwa ahadi kuwa watawapatia fedha kidogo pindi watakapopata mikopo hiyo,alisema jambo hilo ni kosa la kisheria la kula nyama kuitapeli serikani na wakibainika watachunguzwa na kufikishwa katika vyombo vya sharia.Aidha alihimiza vikundi vilivyokopa awali ambavyo hawasilisha marejesho yao warejeshe mapema kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.Ailiwataka wananchi wananufaika /wanaotarajia kunufaika na mikopo hiyo kuzingatia kanuni sharia na taratibu za serikali katika kuomba na kunufaika na mikopo hiyo inayotolewa na Halmashauri kwa vikundi vya Vijana Wanawake na Watu wenye Ulemvu.
Meneja wa Benki ya NMB wa Tawi la Simanjiro.
Meneja wa Benki wa Tawi la Simanjiro aliwahimiza wananchi wenye vigezo kuchangamkia fursa ya Mikopo hiyo ya Masharti nafuu na isiyo na riba ili kuweza kuanzisha miradi mbalimbali ya Ujasirimali itakayowakwamua kutoka katika hali ya umasikini na utegemezi.
Aidha alisema benki yake inashirikiana na Halmashauri katika kutoa elimu ya ujasiriamali ,pamoja na utunzaji wa kumbukumbu za fedha ili wanufaika hao wapate tija kutoka katika mikopo hiyo pamoja na kuweza kurejesha pesa walizokopa .
Aidha alisema kuwa benk yake iko tayari kusaidia ufunguaji wa akaunti kwa haraka kwa vikundi vinavyoanzishwa.
MNUFAIKA:
Mnufaika wa mikopo ya kikundi cha wanawake Nakweni.
Pia Mnufaika Mwingine Bw.Daniel alihimiza vijana na wanawake kuungana pamoja ili kupewa mikopo itakayowasaidia katika shughuli zao za ujasiriamali .Aidha Bw.Daniel alieleza kuwa mkopo waliopata wa shilingi milioni tatu katika kikundi chao cha Enaboishu waliutumia kununua mbuzi 53 na kuwanenepesha na kuwauza kwa faida ,hivyo waliweza kupata fedha za marejesho ya mkopo huo wote na kubakiwa na akiba ambayo waliitumia kwa shughuli zao mbalimbali za maendeleo na kujikwamua kiuchumi.
Mnufaika huyo Bw.Daniel aliwahimiza wanawake na vijana kukuungana na kukopa fedha hizo kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza miradi watakayoibuni.
Makamu Mwenyekiti wa Wilaya ya Simanjiro Mh Sendeu Laizer.
Makamu Mwenyeki wa Wilaya ya Simanjiro .Mh Sendeu lazier alisema kuwa Halmashauri yake chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Halmshauri Mh.Baraka Kanunga lazier itaendelea kukusanya fedha kwa bidii na kutoa asilimia kumi kwa ajili ya Mikopo ya Vikundi vya vijana ,Wanawake na watu wenye lulemavu.
Aliwataka wanufaika wa mikopo hiyo kutoka kata mbalimbali za Wilaya ya Simanjiro kutumia fedha hizo vizuri ili wapate faida pamoja na marejesho ya fedha hizo walizopata kama faida katika shughuli mbalimbali za maendeleo yao ikiwa ni hatua ya kujikwamua kutoka katika hali ya umasikini.
Mkurugenzi:
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya Bw. Gasto.S. Silayo aliipongeza idara ya Maendeleo ya jamii kwa kuwahudumia wananchi kwa kuwapatia mikopo vikundi mbalimbali vya wanawake vijana na watu wenye ulemavu waliopatiwa mikopo isiyo na riba kutoka Halmashauri.
Aidha aliendelea kusema kuwa Halmashauri itaendelea kukusanya mapato zaidi ili kuweza kupata fedha za kuwakopesha vikundi hivyo na kuwakwamua wananchi kutoka katika hali ya umasikini.
Alimkaribisha Mkuu wa Wilaya ili kuongea na wananchi kutoka katika vikundi mbalimbali vilivyopo Wilayani Simanjiro vilivyonufaika na Mikopo hiyo ya Masharti nafuu na isiyo na riba inayotolewa na Halmashauri kwa vikundi mbalimbali vya Vijana Wanawake na Watu wenye ulemavu.
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mh.Dr Suleiman Serera.
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ailiipongeza kamati ya huduma za jamii, Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa kazi nzuri wanayoifanya aidha aliigiza kamati hiyo kukaa vikao vyake kwa wakati ili fedha hizo kwa ajili ya mikopo ya wanawake vijana na watu wenye ulemavu itoke kwa wakati.Pia aliihimiza idara ya maendeleo ya jamii kutoa elimu zaidi ya fedha ,ujasiriamali ,utunzaji wa kumbukumbu za fedha na uongozi kwa wanavikundi ili waweze kutumia mikopo yao kwa tija na kuweza kurejesha marejesho yao kwa wakati.
Aidha alimuagiza mkurugenzi kumpelekea orodha ya vikundi ambavyo havijawasilisha marejesho yao ili aweze kuvifuatilia na kupata fedha za kukupesha vikundi vingine.
“Simanjiro yetu itajengwa na sisi sote”
copyright@2016 Halmashauri ya Wilaya Simanjiro.Haki zote zimehifadhiwa