• Email za Serikali |
    • Malalamiko |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Mawasiliano |
    • Mifumo |
Simanjiro District Council
Simanjiro District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro

  • Mwanzo
  • About us
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Administration
    • Muundo wa Halmashauri
    • Sehemu
      • Infastructure,Rural and Urban Development
        • Works
        • Roads
        • Rural & Urban Development
      • Health,Social Walfare & Nutrition Services
        • Health Services
        • Nutrition Services
        • Social Walfare
      • Industry ,Trade and Investment
        • Industry Development & Investment
        • Trade & Marketing
      • Pre-Primary & PPrimary Education
        • Academics
        • Special Needs Education
        • Adult & Non Formal Education
      • Seconadry Education
        • Academics
        • Statistics & Logistics
        • Special Needs
        • Adult & Non Formal Education
      • Community Development
        • Cross-Cutting Issues Cordination
        • Ngos's & Cbos's Coordination
      • Agriculture,Livestock and Fisheries
        • Agriculture
        • Livestock
        • Fisheries
      • Administration & Human Resources Management
        • Human Resource Management
        • Utawala
      • Planning and Coordination
        • Planning and Budgeting
        • Monitoring and Evaluation
      • LGA'S LAND ADMINISTRATION OFFICE-Ministry of Land ,Housing and Humman Settlement
    • Vitengo
      • Sports,Culture & Arts
      • ICT Unit
      • Government Communication Unit
      • Waste Management & Sanitation Unit
      • Legal Services Unit
      • Internal Audit Unit
      • Procurement Management Unit
      • Natural Resources & Environment Unit
      • Finance & Accounts Unit
  • Fursa za Uwekezaji
    • Madini
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Utoaji wa Leseni za Biashara
    • Utoaji wa Lesseni za Vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa Leseni Za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya Asilimia Kumi(10%)
    • Upimaji wa Ardhi
    • Usajili wa Vikundi vya Kijamii
    • Uandikishaji wa Bima ya Afya ya Jamii(iCHF)
    • Utoaji wa Vitambulisho vya Wajasiriamali Wadogo
    • Kulipia Tozo Za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Huduma za Halmashauri
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
    • Suku ya Kumwona Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Report
    • Vipeperushi
    • Miongozo Mbalimbali
    • By Laws
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Hotuba

Mkutano wa wadau kuhusu utoaji wa maoni ya Dira ya Maendeleo ya mwaka 2050

Imetumwa lini: July 29th, 2024

Katibu Tawala Wilaya ya Simanjiro Bi.Warda A. Maulid aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mh. Fakii R. Lulandala alifungua na kuendesha mkutano wa wadau kuhusu utoaji wa maoni ya Dira ya Maendeleo ya Miaka 25 ijayo yani Dira ya maendeleo ya mwaka 2050 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro tarehe 29.7.2024.Katika  Mkutano huo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Dr. Swaleeh Masaza alitoa mwongozo wa Utoaji wa maoni kwa kuwaeleza washiriki kuanza kutoa maoni juu ya mafanikio na changamoto na utatuzi wa changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025. Wajumbe walitoa maoni yaona kukubaliana kuwa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025 yani Dira ya 2000-2025 imekuwa na Mafanikio yafuatayo -;

Katika swala la Jamii iliyoelimika na kujifunza kuna mabadiliko makubwa.  Pamoja na Sera nzuri ya elimu, wajumbe walieleza kuwa ufundishaji wa wanafunzi mashuleni bado una changamoto kutokana na jamii kuhamasika na Sera ya elimu bila malipo na kupelekea upungufu wa walimu na miundombinu.

Aidha katika suala la Utawala na Uongozi bora mafanikio yaliyopatikana yalikuwa makubwa mno.

Pia lengo la Amani na utulivu limefanikiwa kwa asilimia kubwa kwani nchi yetu hadi sasa ina amani na utulivu tele.

Vilevile, Suala la Maisha Bora na Mazuri ni swala mtambuka kwasababu linalenga mtu mmoja mmoja, lakini kwa ujumla maisha yamebadilika na kuwa ni mazuri.

Uchumi Imara na wenye kuhimili Ushindani umefanikiwa kwa kiasi kidogo kwa kuwa hali za uchumi kwa jamii ya kifugaji bado haijaimarika.

Wadau wa Mandeleo pamoja na Wananchi walieleza Changamoto zilizojitokeza katika Utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025 kama ifuatavyo: 

Mporomoko wa maadili katika jamii.

Kuwepo kwa migogoro mingi hasa migogoro ya ardhi

Uhaba wa miundombinu ya barabara, madarasa na mabweni

Usimamizi wa miradi ya maendeleo iliyoanzishwa katika jamii usioridhisha

Uhaba wa ajira hasa katika kada ya walimu (Upungufu wa Walimu shuleni)

Viongozi wachache kutokua na maadili katika usimamizi wa shughuli za Serikali.

Maeneo mengi ya miji kutopimwa. (Mfano: Orkesumet na Mirerani)

Wadau wa Mandeleo pamoja na Wananchi walieleza Utatuzi wa Changamoto zilizojitokeza katika Utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025 kama ifuatavyo: 

Kuanzishwa kwa mabaraza ya wazee, Ziara ya viongozi zimendelea kufanyika mara kwa mara ili kubaini changamoto na vipaumbele vya wananchi katika maeneo yao, Taratibu za ugawaji wa ardhi zizingatiwe ili kuepuka uibukaji wa migogoro ambayo inarudisha maendeleo nyuma kwa mtu mmoja mmoja na jamii nzima kwa ujumla, Huduma muhimu zisogezwe kwa jamii, mfano umbali kati ya makazi na shule unasababisha changamoto ya kuwepo na wimbi la jamii isiyoweza kusoma na kuandika, Uanzishwaji wa viwanda vya usindikaji wa ngozi kutokana na rasilimali ya mifugo iliyopo katika wilaya ya Simanjiro ufanyike, Kuruhusu na kukaribisha wawekezaji kutoka nje, Kutenga maeneo ya kuweza kuanzisha huduma za kidini. Mfano uanzishwaji wa kanisa ambalo litaanzisha shule za chekechea na kulea jamii katika maadili mema, Jamii iruhusiwe kuanzisha upatikanaji wa huduma muhimu kama maji kwa kuruhusiwa kuchimba visima binafsi, Adhabu kali itolewe kwa wahusika watakaobainika katika kosa la kukatisha masomo ya wanafunzi kwa ajili ya mimba ili jamii iweze kujifunza, Jamii ihamasike na kuchangia gharama za kuwalipa walimu wa kujitolea ili kutatua changamoto ya uhaba wa walimu, Tafiti zifanyike na maandiko yaandaliwe na kuyawasilisha kwa wahusika na kuwakaribisha wawekezaji kutoka nje, Elimu ya ujasiriamali itolewe mashuleni ili kuijengea jamii uwezo wa kujitegemea.







Kadhalika katika dira ya maendleo ya mwaka  2025-2050 wadau na wananchi hao walipendekeza baadhi ya mambo yanayotakiwa kufanyika kama ifuatavyo-;

Kuwepo kwa mwendelezo wa utekelezaji wa Dira kwa kila awamu inayoingia madarakani, Elimu ya Ujasiriamali iwepo shuleni kuanzia shule ya msingi, Serikali isimamie utekelezaji wa sera za bei elekezi ya mazao ili kilinda maslahi ya wakilima.Mfumo wa elimu uendane na dhana ya kujiajiri ili kuwajengea wahitimu waweze kujiajiri, Vyama vya ushirika vifanyiwe maboresho ili kulinda maslahi ya mkulima na wafugaji,Ruzuku ya pembejeo itolewe kwa wakulima na wafugaji,Jamii ishirikishwe katika kutekeleza na kuchangia miradi ya maendeleo, Utamaduni uendelee kuzingatiwa,Jamii izingatie taratibu za uuzaji wa ardhi na uhamishaji wa umiliki ili kuepuka migogoro ndani ya jamii,

Pawepo na uwazi na haki katika swala zima la ajira, Mfumo mzuri wa kuhifadhi mazao ya wakulima kwa lengo la kuboresha uchumi wa wakulima na wafugaji na kuwa na uhakika wa chakula kwa Taifa uaandaliwe, Baraza la Wazee liboreshweKuangalia namba ya kuajiri  walimu wa dini katika kila shule ikiwa ni katika kudumisha maadili

Mwisho Kikao kilifugwa baada ya wadau kuwasilisha mapendekezo hayo, Mwenyekiti wa Halmashauri alipata nafasi ya kusema neno la mwisho katika kikao hicho na alisema kuwa anawasisitiza wananchi wanaoishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro kutumia fursa hii iliyotolewa na serikali kuchangia maoni yao juu ya kitu kinachopaswa kufanyika katika Dira ya Maendeleo ya miaka 25 inayokuja yani Dira ya Maendeleo ya mwaka 2050, Pia alitumia nafasi hiyo Kumpongeza Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Samia Suluhu Hassan  kwa kufanikisha na kusimamia kwa asilima kubwa malengo yaliyowekwa katika Dira ya mwaka 2000-2025,

Kikao kilifugwa Rasmi kwa katibu Tawala wa Wilaya ya Simanjiro Bi.Warda Maulid kwa kuwashukuru na kuwapongeza wananchi na wadau wa maendeleo kwa kujitokeza kwa wingi kuhudhuria kikao hicho na kutoa maoni yao ya nini kifanyike katika Dira ya Maendeleo ya mwaka 2050 na alifunga kikao kwa kuwataka wananchi kutoa maoni yao kwa kutumia njia mbalimbali zilizopendekezwa na serikali ikiwemo kutumia mitandao ya kidigitali na  njia za simu kutoa maoni yao kuhusu dira hiyo.

Alihitimisha kwa kusema kuwa Mwananchi mmoja mmoja anaweza kutoa maoni kupitia:online portal ya https://dira2050portal.planning.go.tz/tume/dira Au

Kutoa maoni kupitia simu za mkononi USSD *152*00# aende Na. 8 - Elimu then Na. 4 – Dira 2050

#Kwa pamoja Tujenge Tanzania Tuitakayo.

Matangazo

  • Wanafunzi waliochaguliwa Shule za Vipaji maalumu,Ufundi,Bweni kawaida na shule maalumu 2023 December 14, 2022
  • wavulana waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2023 simanjiro day schools December 14, 2022
  • wasichana waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2023 Wilaya ya Simanjiro day schools December 14, 2022
  • Tangazo la Ajira Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro May 23, 2022
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • Nyerere day

    October 14, 2024
  • Mkutano wa wadau kuhusu utoaji wa maoni ya Dira ya Maendeleo ya mwaka 2050

    July 29, 2024
  • MWENGE WA UHURU

    July 16, 2024
  • Kifo Cha Raisi awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi 2024

    February 29, 2024
  • Ona vyote

Video

Mh.Dr Serera azindua kipindi cha Pili awamu ya Tatu ya TASAF Wilayani Simanjiro
video Zaidi

Fika kwa Haraka

  • Government Mailing System
  • Mission and Vision
  • Organization Structure
  • Completed Projects

Kiungo Muunganisho

  • Ikulu
  • Utumishi
  • Matokeo kidato cha sita 2021
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Idara ya Habari-Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Government Mailing System

copyright@2016 Halmashauri ya Wilaya Simanjiro.Haki zote zimehifadhiwa