• Email za Serikali |
    • Malalamiko |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Mawasiliano |
    • Mifumo |
Simanjiro District Council
Simanjiro District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro

  • Mwanzo
  • About us
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Administration
    • Muundo wa Halmashauri
    • Sehemu
      • Infastructure,Rural and Urban Development
        • Works
        • Roads
        • Rural & Urban Development
      • Health,Social Walfare & Nutrition Services
        • Health Services
        • Nutrition Services
        • Social Walfare
      • Industry ,Trade and Investment
        • Industry Development & Investment
        • Trade & Marketing
      • Pre-Primary & PPrimary Education
        • Academics
        • Special Needs Education
        • Adult & Non Formal Education
      • Seconadry Education
        • Academics
        • Statistics & Logistics
        • Special Needs
        • Adult & Non Formal Education
      • Community Development
        • Cross-Cutting Issues Cordination
        • Ngos's & Cbos's Coordination
      • Agriculture,Livestock and Fisheries
        • Agriculture
        • Livestock
        • Fisheries
      • Administration & Human Resources Management
        • Human Resource Management
        • Utawala
      • Planning and Coordination
        • Planning and Budgeting
        • Monitoring and Evaluation
      • LGA'S LAND ADMINISTRATION OFFICE-Ministry of Land ,Housing and Humman Settlement
    • Vitengo
      • Sports,Culture & Arts
      • ICT Unit
      • Government Communication Unit
      • Waste Management & Sanitation Unit
      • Legal Services Unit
      • Internal Audit Unit
      • Procurement Management Unit
      • Natural Resources & Environment Unit
      • Finance & Accounts Unit
  • Fursa za Uwekezaji
    • Madini
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Utoaji wa Leseni za Biashara
    • Utoaji wa Lesseni za Vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa Leseni Za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya Asilimia Kumi(10%)
    • Upimaji wa Ardhi
    • Usajili wa Vikundi vya Kijamii
    • Uandikishaji wa Bima ya Afya ya Jamii(iCHF)
    • Utoaji wa Vitambulisho vya Wajasiriamali Wadogo
    • Kulipia Tozo Za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Huduma za Halmashauri
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
    • Suku ya Kumwona Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Report
    • Vipeperushi
    • Miongozo Mbalimbali
    • By Laws
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Hotuba

Baraza la kata H/W Simanjiro July-Sept 2023

Imetumwa lini: October 23rd, 2023

Kikao cha baraza la kata la Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro kiliketi mnamo tarehe 23-October -2023 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Simanjiro.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro,Katibu tawala wa Willaya ya Simanjiro,Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Simanjiro,Makatibu tarafa kutoka tarafa mbalimbali za Wilaya ya Simanjiro,Wataalamu kutoka idara mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro,Wataalamu kutoka taasisi mbalimbali zilizopo katika Wilaya ya Simanjiro .

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mh.Baraka Kanunga Laizer alifungua kikao kwa salamu kisha aliwataka waheshimiwa madiwani wawasilishe taarifa za utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za kiserikali kutoka katika kata zao zilizotekelezwa kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/2024(July-September 2023).Baadhi ya taarifa hizo  ni Utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika kata husika,Hali ya usalama katika kata husika , tarifa za kilimo na mifugo katika kata husika,mgawanyo wa watumishi wa serikali katika kata husika,changamoto zinazokabili kata husika Pamoja na mafanikio yaliyopatikana  katika kata husika.Baadhi ya taarifa zilizowasilishwa na waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro ni kama zinavyoonekana hapo chini.

 

 

MIRERANI

Katika kipindi cha July-September 2023Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikeleza miradi ifuatayo katika kata ya Mirerani:-

  • Utengenezaji wa Barabara ya lami kutoka Barabara kubwa Getini hadi kwenye Geti la Magufuli fedha kutoka Serikali kuu kupitia TARURA wilaya ya Simanjiro.
  • Utengenezaji wa viti na meza 77  za wanafunzi katika shule ya sekondari Tanzanite kwa gharama za shilingi 5,000,000/=  fedha zilizotoka katika mfuko wa Jimbo

Aidha Diwani wa Kata ya Mirerani alisema kuwa kata hiyo bado inakabiliwa na changamoto za uhaba wa nyumba za walimu,Uhaba wa madarasa kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi katika shule zilizopo kata ya Mirerani ,miundombinu  iliyoharibika ya Barabara kutoka sheli ya kibobo kuelekea Losoito(Emishiye) kata ya Naisinyai ,Pia aliiomba halmashauri ipime eneo kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama .

ORKESUMET

 

Aidha katika kata ya Orkesumet diwani wa kata hiyo Mh.Sendeu laizer  alisema kuwa serikali ilitekeleza na  inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali katika kata hiyo ,Baadhi ya miradi hiyo ni Ujenzi wa Barabara za mji wa Orkesumet km 14.6 kwa kiasi cha shilingi milioni mia moja na kumi na tisa 119,000,000 kupitia TARURA,Ujenzi wa Barabara ya kiwango cha lami KM 1.01 kwa gharama ya shilingi milioni mia sita( 600,000,000/=).

Aidha kupitia Mradi wa Utunzaji wa Mazingira  EBBAR serikali inaendelea kutekeleza miradi ifuatayo chini usimamizi wa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro;

  • Uwekaji wa miundombinu ya visima viwili kwa gharama ya shilingi 54,000,000(Milioni Hamsini na nne)
  • Ujenzi wa vitalu nyumba katika mitaa ya jitegemee na Mkumbi kwa gharama ya shilingi 42,348,000/=
  • Mradi wa kununua ng’ombe na mbuzi wa maziwa kikundi cha Mkumbi kwa gharama ya shilingi milioni sitini na tano (65,000,000/=)
  • Mradi wa ufyatuaji wa matofali katika kikundi cha Mkumbi kwa gharama ya shilingi milioni ishirini(20,000,000/=)
  • Uchakataji wa chakula cha Mifugo katika kikundi cha Mkumbi kwa gharama ya shilingi milioni ishirini(20,000,000/=)
  • Ununuzi wa mbuzi wa maziwa katika kikundi cha jitegemee kwa gharama ya shilingi milioni ishirini(20,000,000/=).
  • Mh.Sendeu alihitimisha kwa kuipongeza serikali kupitia viongozi wake kwa  kutenga na kuleta fedha hizo katika kata yake na kuiomba halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro kuharakisha utoaji wa fedha hizo ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati.
  •  
  • EMBOREET
  • Mh.Yohana Shinini (Diwani wa kata ya Emboreet) alisema kuwa katika kipindi cha mwenzi July hadi September 2023  serikali imekamilisha miradi ifuatayo kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro;
  • Ujenzi wa madarasa matatu na choo cha shule ya Msingi Mbuko kwa fedha kutoka Serikali kuu kupitia mradi wa BOOST kiasi cha shilingi milioni themanini na moja na laki tatu(81,300,000/=)
  • Mradi wa kuzungusha fensi katika  zahanati ya Loiborsoit  “A”
  • Aidha alisema kuwa shirika la Eclat Foundation  limechangia ujenzi  wa tanki kubwa la kuhifadhia  maji lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita elfu sitini(60,000) katika shule ya Msingi Pendo Lenaitunyo.
  • Mh.Diwani alliiomba halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro kupeleka fedha katika kata hiyo ili kumalizia miradi ya Ujenzi wa madarasa matatu katika shule shikizi Losesia kwani ujenzi wa madarasa matatu ya shule hiyo umesimama katika hatua ya Msingi,Ujenzi wa Nyumba ya Walimu “Two-in -One” katika shule ya Msingi mbuko  iliyofikia katika hatua ya lenta,Ujenzi wa matundu 17  ya vyoo katika shule ya Msingi Osilalaei ambako ujenzi huo umesimama katika hatua ya plasta,Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja katika shule ya awali Meleleki  ambako ujenzi umesimama katika hatua ya upauzi.
  • Aidha Mh.Diwani alikumbushia ombi la wananchi na mfadhili wa Shule ya Msingi Pendo-Lenaitunyo kubadilishwa mtaala wa Kiswahili na kufundisha kwa mtaala wa kiingereza(English Medium).
  • NABERERA
  • Kata ya Naberera serikali imekamilisha ujenzi wa miradi ifuatayo:
  • Ujenzi wa shule ya Msingi Lengijape kwa gharama ya shilingi 638,300,000 /= fedha kutoka serikali kuu.
  • Ujenzi wa nyumba ya watumishi wa Afya katika Kijiji cha losokonoi
  • Aidha aliiomba halmashauri kutenga na kupeleka fedha katikia kata hiyo ili kukamilisha miradi ifuatayo:
  • UUjenzi wa darasa moja katika shule ya Msingi lolbene uliokwama katika hatua ya msingi.
  • Aidha alisema kuwa kata hiyo inakabiliwa na magonjwa ya mifugo ya ndigana baridi,Ndigana kali,Kutupa mimba kwa ng’ombe na mbuzi,ugonjwa wa Sokota na homa ya Mapafu.
  • Pia alisema kuwa kata ya Naberera imefanikiwa kupata fedha zifuatazo kutoka Serikali kuu na Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro katika kipindi cha mwnzi July hadi September 2023 .
  • Kiasi cha shilingi milioni Hamsini (50,000,000) kwa ajili ya  ujenzi wa madarasa
  •  mawili katika shule ya Msingi Naberera.
  • Shilingi Milioni Hamsini nna moja na laki tano (51,500,000/=) kwa ajili ya uboreshaji wa zahanati ya Okutu.
  • Shilingi milioni kumi na moja  kwa ajili ya matundu nane ya vyoo shule shikizi ya Ormotii.
  • Shilingi milioni mbili na laki nne (2,400,000/=)  kutoka Mfuko wa Jimbo kwa ajili ya kumalizia nyumba ya Waalimu katika shule shikizi ya Ormoti.
  • Shilingi milioni tano (5,000,000) kutoka mfuko wa jimbo kwa ajili ya kumalizia nyumba ya waalimu katika shule shikizi ya Kidomungen
  • Shilingi milioni kumi kutoka mfuko wa jimbo kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Zahanati ya Lorbene
  • KOMOLO

Katika kata ya komolo Serikali,Halmashauri ya Wafadhili wa mekamilisha miradi ifuatayo:

  • Ujenzi wa shule ya Msingi Acronis inayojengwa na Shirika la Eclat Foundation.
  • Ujenzi wa ofisi ya Kijiji cha Kitiangare
  • Ujenzi wa darasa la chekechea kitongoji cha Mang’eeny
  • Ujenzi wa kituo cha Afya komolo majengo mawili yamekamilika na umegharimu fedha kiasi cha shilingi 330,561,162.67 zilizotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro.
  •  
  • KITWAI
  • Mh.Diwani wa kata ya kitwai alisema kuwa katika kata yake miradi mbalimbali ya maendeleo imetekelezwa kwa fedha kutoka serikali kuu na Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro.Baadhi ya miradi hiyo ni Pamoja na :
  • Ujenzi wa majengo mapya kumi katika shule ya sekondari kitwai unaogharimu kiasi cha shilingi 584,280,028.00
  • Ujenzi wa madarasa mawili shule ya msingi Loondrekes kwa gharama za shilingi 31,250,000/=.
  • Ukarabati wa wodi ya wajawazito Zahanati ya kitwai  kwa gharama za shilingi 36,000,000/=.
  • Mh.diwani wa kata hiyo aliiomba Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro iharakishe utatuzi wa mgogoro wa ardhi  baina ya kata hiyo na Wilaya Jirani  ya Kilindi .
  • RUVU REMIT
  • Katika kipindi cha Mwenzi July hadi September 2023 Kata ya Ruvu Remit  imetekeleza miradi ya maendeleo ifuatayo;
  • Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa kwa kiasi cha shilingi milioni Hamsini(50,000,000/=) fedha kutoka serikali kuu.
  • Ujenzi wa josho la kuogeshea Wanyama katika Kijiji cha lerumo mradi uliogharimu kiasi cha shilingi milioni ishirini na sita(26,000,000/=)
  • Ujenzi wa josho la kuogeshea Wanyama katika Kijiji cha gunge mradi uliogharimu kiasi cha shilingi milioni ishirini na sita(25,800,000/=)
  • Aidha aliiomba halmashauri imsadie katika upanuzi wa nyumba ya waalimu katika shule shikizi ya Irkirinen iliyojengwa kwa  nguvu za wananchi,kuongeza waalimu katika shule ya msingi Ruvu-Remit na uendelezaji wa mfereji wa umwagiliaji wa Noorkimbey-Olbili.

NGORIKA

Katika kata ya Ngorika serikali imetekeleza miradi ya ujenzi wa nyumba ya Waalimu ambayo imefikia hatua ya umaliziaji  hivyo aliimba Halmashauri imalizie kuwagawia kiasi cha shilingi milioni saba kutoka katika mapato ya ndani ya Halmashauri  kwa ajili ya ukamilishaji,Ujenzi wa Matundu nane ya vyoo katika shule ya msingi Lengumwuna uliogharimu kiasi cha sjilingi milioni kumi na moja na kupelewa na kiasi cha shilingi milioni tano na laki tanio kwa ajili ya ukamilishaji.

Ujenzi wa Jiko katika Shule ya Sekondari Nyumba ya mungu ambao unaendelea na aliiomba halmashauri kupeleka kiasi cha shilingi milioni kumi katika shule hiyo ili kukamilisha mradi huo wa ujenzi wa jiko.

Aidha aliiomba halmashauri kupitia mapato yake ya nadani kuchangia ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa kupitia mapato ya nadani ya Halmashauri ili kuunga mkono jitihada za wananchi.

Akidha aliipongeza Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) kwa kupanua mradi na kujenga tank la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 150,000 ambapo ujenzi huo unaogharimu kiasi cha shilingi milioni mia moja na sitini na tano(165,000,000/=)  unaendelea,Pamoja na uchimbaji wa visima kambi ya chui na Lengungumwa.

Aidha alisema kuwa Kata yake imetenga na kusafisha eneo kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya hivyo anaiomba Halmashauri kutenga pesa kwa ajili ya Kuanza ujenzi wa kituo hicho ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za Afya kwa wananchi wa kata ya Ngorika badala ya Kwenda Mkoa wa Kilimanjaro katika Hospitali za KCMC na Mawenzi ambapo hutumia gharama kubwa za usafiri na kusafiri umbali mrefu.

Aidha aliiomba TARURA Kukarabati Barabara ya NGAGE-NYUMBA YA MUNGU-KISANGARA kwani Barabara hiyo ina maeneo mengi korofi hivyo kudhoofisha hali ya uchumi na huduma za kijamii katika kata hiyo.Pia aliiomba TARURA kukarabati kivuko cha Kagera ambacho hakipitiki wakati wa kipindi cha mvua.Pia aliiomba halmashauri kuweka doria Pamoja na kushirikiana na Wilaya Jirani ya Mwanga kudhibiti uvuvi haramu  ,kupiga marufuku shughuli za kibinadamu kandokando ya bwawa la Nyumba ya Mungu,kukopesha vikundi vya wavuvi ili wanunue nyenzo zinazokubalika kwa uvuvi,kupiga marufuku na kutoza faini kwa uuzaji wa Samaki wachanga sokoni,kutoa leseni za uvuvi kwa kuzingatia sheria za uvuvi Pamoja na kutoa elimu ya namna ya kuboresha uvuvi kwa kuanzisha  uvuvi wa vizimba nnje ya bwawa.

KATA YA LOIBORSOIT

Mh.Diwani wa kata ya Loiborsoit alisema kuwa katika kata yake serikali imetoa kiasi cha shilingi 19,990,000 kwa ajili ya kuboresha skimu ya umwagiliaji Ngage.

Idha aliwaomba maafisa mifugo wa Wilaya kuhamasisha wafugaji kuchanja mifugo yao ili kuzuia madhara makubwa yatokanayo na ugonjwa wa SOTOKA

Aidha alisema kuwa kata yake inakabiliwa na ubovu wa miundombinu ya Barabara kutoka mashambani kwa ajili ya kusafirisha mazao yanayolimwa  Kwenda sokoni.Pia alishauri Idara ya kilimo kutoa kwa wakati pembejeo zinazotolewa na serikali ili wakuliwa waweze kuzipata kwa bei nafuu.Aidha alisema kuwa kata yake ina upungufu mkubwa wa waalimu wa kike katika shule za msingi Loiborsoit ‘B”,ndepesi na Mazinde.Pia aliomba TANESCO kufikisha huduma ya Umeme katika maeneo ya Ndepesi,Jangwani,kwasakwasa na Mangulai mwisho aliomba Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro kutenga  fedha katika baject ijayo ili kuwezesha ujenzi wa Josho la Kuogeshea Wanyama kwani mifugo mingi inaathirika na magonjwa yanayosababishwa na kupe.

NAISINYAI

Mh.Diwani wa kata ya Naisinyai alisema kuwa katika kipindi cha Robo ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2023/2024  kata ya Naisinyai ilipata kiasi cha shilingi milioni mia moja na thelathini( 130,000,000/=) kutoka serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa bweni moja katika shule ya Sekondari Naisinyai ,Pia kata ya Naisinyai ilipata kiasi cha shilingi  milioni thelathini  (30,000,000/=)  kutoka mgodi wa FRANONE kwa ajili ya umaliziaji wa nyumba ya waalimu “two-in -one”

Aidha Mh.diwani aliiomba Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro kuchangia fedha kwa ajili ya ununuzi wa vitanda na madawati kwani kuna ongezeko la wanafunzi 502 wa kidato cha Tano katika shule ya sekondari Naisinyai.

Pia aliiomba TANESCO kufikisha huduma ya umeme katika kisima kilichochimbwa kwa ajili ya kuhudumia shule hiyo ili kuwezesha usukumaji wa maji kuelekea maeneo ya shule hiyo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Simanjiro Mh.Baraka Kanunga Laizer aliipongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Mh.Samia Suluhu Hasan kwa kutenga na kuleta fedha za kutekeleza Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro ,pia alimpoongeza Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mh.Dr Suleiman Serera ,Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mh.Ole Sendeka ,Katibu tawala wa Wilaya ya Simanjiro ,Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro ,wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Pamoja na wataalamu kutoka katikaTaasisi za kiserikali na kibinafsi zilizopo katika wilaya ya simanjiro ,viongozi wa serikali za mitaa na vijiji Pamoja na wananchi wote wa Wilaya ya Simanjiro kwa kushiriki na kusimamia Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro,Pia alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro kushughulikia kwa haraka  maoni ,kero na mapendekezo yote yaliyowasilishwa na waheshimiwa madiwani wa kata za Halmashauri ya Wilaya ya simanjiro.Mwisho aliahirisha kikao hicho  cha baraza la kata mpaka robo ya pili yam waka wa fedha 2023/2024.


“Kazi iendelee……………………………….”

Matangazo

  • Wanafunzi waliochaguliwa Shule za Vipaji maalumu,Ufundi,Bweni kawaida na shule maalumu 2023 December 14, 2022
  • wavulana waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2023 simanjiro day schools December 14, 2022
  • wasichana waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2023 Wilaya ya Simanjiro day schools December 14, 2022
  • Tangazo la Ajira Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro May 23, 2022
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • Nyerere day

    October 14, 2024
  • Mkutano wa wadau kuhusu utoaji wa maoni ya Dira ya Maendeleo ya mwaka 2050

    July 29, 2024
  • MWENGE WA UHURU

    July 16, 2024
  • Kifo Cha Raisi awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi 2024

    February 29, 2024
  • Ona vyote

Video

Mh.Dr Serera azindua kipindi cha Pili awamu ya Tatu ya TASAF Wilayani Simanjiro
video Zaidi

Fika kwa Haraka

  • Government Mailing System
  • Mission and Vision
  • Organization Structure
  • Completed Projects

Kiungo Muunganisho

  • Ikulu
  • Utumishi
  • Matokeo kidato cha sita 2021
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Idara ya Habari-Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Government Mailing System

copyright@2016 Halmashauri ya Wilaya Simanjiro.Haki zote zimehifadhiwa