• Email za Serikali |
    • Malalamiko |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Mawasiliano |
    • Mifumo |
Simanjiro District Council
Simanjiro District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro

  • Mwanzo
  • About us
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Administration
    • Muundo wa Halmashauri
    • Sehemu
      • Infastructure,Rural and Urban Development
        • Works
        • Roads
        • Rural & Urban Development
      • Health,Social Walfare & Nutrition Services
        • Health Services
        • Nutrition Services
        • Social Walfare
      • Industry ,Trade and Investment
        • Industry Development & Investment
        • Trade & Marketing
      • Pre-Primary & PPrimary Education
        • Academics
        • Special Needs Education
        • Adult & Non Formal Education
      • Seconadry Education
        • Academics
        • Statistics & Logistics
        • Special Needs
        • Adult & Non Formal Education
      • Community Development
        • Cross-Cutting Issues Cordination
        • Ngos's & Cbos's Coordination
      • Agriculture,Livestock and Fisheries
        • Agriculture
        • Livestock
        • Fisheries
      • Administration & Human Resources Management
        • Human Resource Management
        • Utawala
      • Planning and Coordination
        • Planning and Budgeting
        • Monitoring and Evaluation
      • LGA'S LAND ADMINISTRATION OFFICE-Ministry of Land ,Housing and Humman Settlement
    • Vitengo
      • Sports,Culture & Arts
      • ICT Unit
      • Government Communication Unit
      • Waste Management & Sanitation Unit
      • Legal Services Unit
      • Internal Audit Unit
      • Procurement Management Unit
      • Natural Resources & Environment Unit
      • Finance & Accounts Unit
  • Fursa za Uwekezaji
    • Madini
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Utoaji wa Leseni za Biashara
    • Utoaji wa Lesseni za Vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa Leseni Za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya Asilimia Kumi(10%)
    • Upimaji wa Ardhi
    • Usajili wa Vikundi vya Kijamii
    • Uandikishaji wa Bima ya Afya ya Jamii(iCHF)
    • Utoaji wa Vitambulisho vya Wajasiriamali Wadogo
    • Kulipia Tozo Za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Huduma za Halmashauri
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
    • Suku ya Kumwona Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Report
    • Vipeperushi
    • Miongozo Mbalimbali
    • By Laws
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Hotuba

MASUALA MTAMBUKA

Saturday 24th, May 2025
@SIMANJIRO



MASUALA MTAMBUKA


0.1   Utangulizi

 Katika mada hii utajifunza masuala mtambuka yanayogusa jamii katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupanga, kuainisha, kutekeleza na kutathimini mipango endelevu ya maendeleo katika jamii. Masuala mtambuka yanaweza kuwa na athari kama hayatazingatiwa vyema mahali pa kazi katika utoaji wa huduma. Hivyo, mada hii inalenga kukuwezesha kuyatambua na kuzingatia masuala hayo katika utoaji wa huduma.

Masuala mtambuka yanajumuisha UKIMWI mahala pa kazi; mazingira; jinsia, na rushwa. Aidha, utajifunza umuhimu wa kutambua na kuzitumia fursa zilizopo katika eneo husika; stadi za maisha na TEHAMA.

Malengo Mahsusi

 

0.2   Utawala Bora

Utawala bora ni utaratibu wa utumiaji wa madaraka ya umma kusimamia rasilimali za nchi katika jitihada za kutumia rasilimali hizo kwa ajili ya kuinua hali ya maisha ya wananchi. Utawala bora ni dhana ya ushirikishwaji wa jamii kwa kuzingatia utawala wa sheria, haki, usawa, uwazi na uwajibikaji ili kufikia maamuzi na kujiletea maendeleo. Aidha, utawala bora ni mfumo muhimu katika kuleta maendeleo endelevu kwa lengo la kupunguza umaskini. Pia, unahusisha mapambano dhidi ya ruhswa.

 

0.2.1    Misingi ya Utawala Bora

Utawala bora umejengwa katika misingi ya demokrasia, utawala wa sheria, haki na usawa, ushirikishwaji wa wananchi, uwajibikaji, uwazi na vita dhidi ya rushwa.

   i).        Demokrasia

Demokrasia ni utaratibu ambao viongozi wa wananchi hupatikana kwa njia ya uchaguzi unaoendeshwa kwa njia ya haki inayompa mwananchi uhuru wa kuchagua kiongozi anayemtaka.

  ii).        Utawala wa Sheria

Kila mtu anapaswa kuzingatia na kuongozwa na Katiba ya nchi, Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo katika maisha binafsi, uhusiano na wengine na utekelezaji wa majukumu binafsi. Pia, utawala bora unatoa haki ya mtu kusikilizwa, kutohusisha upendeleo na kutoa sababu kwa maamuzi yote yanayofikiwa.

 iii).        Haki na Usawa

Unapaswa kufanya maamuzi na kutekeleza majukumu yako kwa kuzingatia haki bila ubaguzi wala upendeleo wa aina yoyote. Kwa kufanya hivyo utajenga imani kwa wananchi na itakuwa rahisi zaidi kwako kupata ushirikiano wao katika harakati za maendeleo na vita dhidi ya umaskini.

 iv).        Ushirikishwaji wa Wananchi

Unapopanga mipango ya maendeleo unapaswa kuwashirikisha wananchi katika maamuzi yote yanayohusu ustawi na maendeleo kupitia vikao vya ngazi mbalimbali kama vile mikutano mikuu ya vijiji, mitaa na Kamati za Maendeleo za Kata (Rejea Ibara ya 8 na 146 ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, na Sera ya Ugatuaji wa Madaraka kwa Umma ya 1998).

  v).        Uwajibikaji na Uwazi

Unapotekeleza majukumu yako ya kazi unapaswa kuzingatia kwamba lengo ni kuwahudumia wananchi na siyo kuwatawala au kuwaburuza. Hivyo, unapaswa kuwa karibu nao kuwapa taarifa sahihi kwa wakati iliyo wazi inayobeba majibu ya kutosheleza na kuridhisha.

0.2.2    Faida za Utawala Bora

Utawala bora una faida nyingi ikiwa ni pamoja na kupunguza rushwa, kuzingatia maoni ya watu na hasa ya wale ambao wapo kwenye mazingira magumu, pia mahitaji ya jamii ya sasa na ya baadae. Hivyo, unapaswa kuhakikisha kuwa maoni na mahitaji halisi ya wateja hasa mahitaji ya makundi yenye mahitaji maalumu yanajumuishwa katika mipango yako ya utoaji huduma.

 

Kisa Mkasa


Makungu ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanzo Mgumu alipata fedha ya kuchimba kisima cha maji katika kijiji cha Songambele kutoka kwa wadau wa maendeleo. Wadau hao walimuomba aharakishe utekelezaji wa mradi ili waweze kupata taarifa ya matumizi ya fedha kwa ajili ya kufunga hesabu za shirika lao. Ili kufanikisha hilo, Mkurugenzi aliwasiliana na kampuni Kijiko Bore Hole Drilling ili wafanye utafiti wa upatikanaji wa maji na hatimaye kuchimba kisima.
Kampuni hiyo ilitekeleza jukumu hilo baada ya kutambulishwa kwa Afisa Mtendaji wa kijiji cha Songambele ambaye ndiye mwakilishi wa Mkurugenzi. Kwa bahati nzuri kampuni hiyo ilifanikiwa kupata maji ya kutosha kwa ajili ya matumizi ya wanakijiji. Kwa furaha Mkurugenzi aliamua kumualika Mkuu wa Mkoa ili azindue mradi na kutumia fursa hiyo kuwasisitiza kuandaa taratibu za kuufanya mradi huo kuwa endelevu.
Baada ya uzinduzi, Mkuu wa Mkoa aliwaruhusu wanakijiji waulize maswali kuhusu mradi na namna ya kuuendesha. Katika hali ya kushangaza wanakijiji waliaanza kwa kuonesha kutoridhishwa na mradi kwa madai kuwa kisima kilichimbwa mbali na maeneo ya makazi yao. Aidha, mwanakijijii mmoja alilalamika kuwa kisima kilichimbwa katika shamba lake bila makubaliano. Kwa ujumla Mkuu wa Mkoa alipata picha kuwa wanakijiji walitaka kuususia mradi. Mkurugenzi alionekana kuchanganyikiwa na kutaka kutoa majibu. Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa alimtaka asijibu na baadala yake afanye uchunguzi ili kupata majibu sahihi juu ya yaliyojitokeza na hatimate kutatua kero za mradi.
Maswali 
Kwa kuwa uliongozana na Mkurugenzi katika uzinduzi huo, Mkurugenzi anakuagiza upitie mchakato mzima wa utekelezaji wa mradi na kutoa ushauri. 
  1. Ni kitu gani kiliwafanya wanakijiji kutoridhika na utekelezaji wa mradi huo?
  2. Ainisha changamoto za utekelezaji wa mradi na kutoa ushauri ya namna ya kukabiliana nazo ili zisijirudie tenakatika miradi mingine.
 

 

0.3    Rushwa na Athari zake

0.3.1    Maana ya Rushwa

Rushwa ni matumizi mabaya ya madaraka ya umma kwa manufaa binafsi. Rushwa inatafsiriwa kuwa ni kitendo cha kuahidi, kutoa, kupokea au kushawishi moja kwa moja au kupitia wakala; kitu chochote cha thamani ili kupindisha utaratibu katika utoaji wa maamuzi. Unapokuwa unashiriki katika vitendo vya rushwa, au kufumbia macho vitendo hivyo, basi tambua kwamba husababisha kudidimiza utoaji wa huduma kwa umma.

0.3.2    Athari za Rushwa

Rushwa ni adui wa haki, hivyo husababisha wananchi kutopata haki za msingi mfano afya, ajira, mikataba ya huduma mbalimbali, uwekezaji na ugawaji wa ardhi.

Kwa ujumla nchi za kusini mwa jangwa la Sahara zinafanya vibaya katika udhibiti wa vitendo vya rushwa. Hata hivyo, Tanzania imechukua hatua kubwa katika mapambano dhidi ya rushwa. Kwa mfano kwa mujibu wa Shirika la Transparency International (2018), Tanzania inashika nafasi ya 99 kati ya nchi 180. Kutokana na juhudi hizo Serikali ilifanikisha kuokoa kiasi cha shilingi bilioni 53.9 kutokana na uchunguzi na operesheni mbalimbali katika mwaka 2016/2017.


Bonyeza kiunga kutazama video inayoonyesha kuhusu kiasi cha fedha kilichookolewa kutokana na udhibiti wa rushwa 

 

1.3.3    Mapambano Dhidi ya Rushwa

Mapambano dhidi ya rushwa yamesababisha kuwe na mabadiliko katika kanuni na taratibu za kazi za Umma ili kuziba mianya ya rushwa. Mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo:

  1. Sheria ya Kupambana na Kudhibiti Rushwa,1971 imefanyiwa mabadiliko ili kuipa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa, madaraka ya upekuzi, kukamata watuhumiwa na mali na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.
  2. Sheria ya Maadili ya Viongozi, Sura ya 389 imefanyiwa marekebisho na kumuwezesha Kamishna wa Tume ya Maadili kuwa na madaraka ya kuchunguza tuhuma kuhusu kiongozi yeyote kutokana na taarifa za wananchi. Aidha, Taasisi imepewa mamlaka ya kuchunguza fedha za viongozi zilizopo benki kwa kibali cha mahakama.
  3. Sheria ya Manunuzi ya Umma, 2011 iliyofanyiwa na marekebisho yake ya mwaka 2016 imeweka utaratibu ulio wazi wa kuziba mianya ya rushwa katika manunuzi ya umma.
  4. Sheria ya Ukaguzi, 2008 ilitungwa ili kuipa uwezo Ofisi ya Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kufanya ukaguzi wa masuala ya fedha
  5. Sheria ya Gharama za Uchaguzi, 2010 ilitungwa kuhakikisha kuna uwazi na udhibiti katika matumizi ya fedha wakati wa chaguzi.
  6. Sheria ya Utumishi wa Umma, 2002 ilitungwa ili kuweka taratibu na uwazi katika mwenendo mzima wa ajira na usimamizi wa utendaji kazi katika sekta ya umma.
  7. Serikali iliandaa na kuanza kutumia Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa na Mpango wa Utekelezaji Awamu ya Tatu (2017-2022).

0.3.4    Mambo ya Kuzingatiwa na Mtumishi wa Umma katika Kupambana na Rushwa

  1. Kuzingatia sheria, taratibu na kanuni (Kanuni za Maadili ya Utumishi wa Umma) katika utoaji wa huduma kwa wateja wa ndani na nje.
  2. Kutokutoa wala kupokea rushwa
  3. Kutoa taarifa juu ya wanaotoa au kupokea rushwa TAKUKURU
  4. Kubainisha maeneo yenye viashiria vya rushwa katika ofisi husika na kuchukua hatua stahiki
  5. Kutunza siri kwa wanaotoa taarifa zinazohusu masuala ya rushwa.

 

Swali la Tafakuri


Utachukua hatua gani iwapo mteja atakupa zawadi yenye thamani kubwa baada ya kumhudumia vizuri na kwa mujibu wa sheria?

 

0.3.5    Mambo ya Kuzingatiwa na Mtumishi wa Umma katika Kupambana na Rushwa

  1. Kuzingatia sheria, taratibu na kanuni (Kanuni za Maadili ya Utumishi wa Umma) katika kutoa huduma kwa wateja wa ndani na nje.
  2. Kutokutoa wala kupokea rushwa
  3. Kutoa taarifa juu ya wanaotoa au kupokea rushwa TAKUKURU
  4. Kubaini maeneo yenye viashiria vya rushwa katika ofisi husika na kuchukua hatua stahiki
  5. Kutunza siri za wanaotoa taarifa zinazohusu masuala ya rushwa.

 

0.4    Masuala ya Jinsia na Makundi yenye Mahitaji Maalumu

Ili kuielewa dhana ya jinsia inavyojadiliwa katika mtazamo wa maendeleo, ni muhimu kujua tofauti kati ya jinsi na jinsia. Jinsi ni neno linalotumika kutofautisha mwanamke na mwanaume kimaumbile. Jinsia ni uhusiano wa kijamii kati ya wanaume na wanawake unaotokana na mtizamo uliojengeka ndani ya jamii husika. Uhusiano huu umejengwa kutokana na imani za kidini, mila na desturi ya jamii husika kuhusu majukumu, haki na nafasi ya kila jinsi katika kaya, jamii na taifa. Mgawanyo huu wa majukumu, haki na nafasi kati ya jinsi hizi mbili hauna usawa kwani unaelemea upande mmoja na hivyo kuathiri maendeleao endelevu ya jinsi zote mbili katika kaya, jamii na taifa kwa ujumla. Kwa vile uhusiano wa kijinsia unatokana na mitizamo ndani ya jamii, uhusiano huu unaweza kubadilishwa ili kuleta usawa.

Uhusiano huu wa jinsia hujitokeza katika mgawanyo wa rasilimali, elimu, na ushiriki katika maamuzi mbalimbali. Kwa ujumla, dhana ya jinsia inahusu usawa katika jamii na ushirikishwaji wa makundi maalumu katika mipango yote ya maendeleo. Makundi haya yanahusisha wanawake, vijana, wazee, watu wanaoishi na ulemavu, watu wanaoishi na virusi vya ukimwi, na watoto.

0.4.1    Umuhimu wa Kujumuisha Jinsia na Makundi yenye Mahitaji Maalum katika Mipango ya Maendeleo

Upo umuhimu wa kujumuisha jinsia na makundi yenye mahitaji maalumu kwenye mipango ya maendeleo kwa sababu zifuatazo;

  • Huchangia kupunguza ubaguzi wa kijinsia;
  • Huzingatia tofauti kati ya wanawake na wanaume;
  • Huweka wanawake na wanaume kuwa kitovu cha uundaji wa programu sera na sheria na uamuzi;
  • Huhakikisha upokwaji wa haki hauendelezwi;
  • Huongeza ufanisi wa vitendo vinavyolenga kuleta mabadiliko.

0.5    Mazingira

Mazingira ni vitu vyote ambavyo humzunguka mwanadamu kama vile maji, miti, milima, mabonde, miamba na kadhalika.

0.5.1    Hali ya Mazingira Tanzania

Hali ya mazingira Tanzania kwa ujumla si ya kuridhisha. Baadhi ya mambo yanayosabisha uharibifu wa mazingira ni pamoja na kulima na kujenga katika vyanzo vya maji, mbuga za wanyama na hifadhi za Taifa. Kadhalika wenye viwanda humwaga taka zenye sumu katika mito na vijito, na watu hutupa taka ovyo.

Athari za uharibifu wa mazingira ni janga linalosababisha umasikini kwani huathiri moja kwa moja shughuli za uzalishaji mali kama vile kilimo, mifugo, viwanda, biashara na maliasili. Vilevile, uharibifu wa mazingira ni chanzo kikubwa cha magonjwa mbalimbali hasa ya kuambukiza kama vile kipindupindu, magonjwa ya tumbo na kuhara.

0.5.2    Wajibu wa Kulinda Mazingira

 Kulinda na kuhifadhi mazingira ni jukumu la kila raia. Mtu yeyote anayeishi Tanzania ni mdau na atawajibika kutunza na kuendeleza mazingira na kutoa taarifa kwa mamlaka husika kuhusu shughuli au jambo lolote ambalo linaweza kuathiri mazingira. (Rejea Kifungu Na. 6 cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Mwaka 2004).

Mtumishi wa umma kama ilivyo kwa wananchi wengine unawajibu wa kutunza na kulinda mazingira katika maeneo yao ya kazi na katika sekta zao, kwa mfano kuzima vifaa vya umeme ambavyo huna matumizi navyo, kufuata taratibu katika kuteketeza vifaa na mitambo ambayo muda wake wa matumizi umemalizika, na kupunguza matumizi ya karatasi.

Angalizo


Mazingira ni suala nyeti hivyo unapaswa kulinda na kuhifadhi mazingira ya maeneo yako ya kazi au unapoishi. Kwa kufanya hivyo utasaidia kuhifadhi mazingira na kuyafanya  kuwa endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.

0.6   Ukimwi Mahala pa Kazi

UKIMWI ni Upungufu wa Kinga Mwilini unaosabishwa na virusi vinavyoshambulia kinga za mwili. Virusi vya UKIMWI hupunguza uwezo wa mwili kujikinga na magonjwa mbalimbali. Hadi sasa UKIMWI hauna chanjo wala tiba.

0.6.1    Njia Kuu za Maambukizi ya UKIMWI

  • Ngono zembe
  • Kutoka kwa mama mjamzito aliye na maambukizi kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua na kunyonyesha;
  • Kuwekewa damu ya mtu mwenye maambukizi ya VVU;
  • Kuchangia vifaa vyenye ncha kali na mtu mwenye maambukizi ya VVU;
  • Kugusana na damu au majimaji ya mwili wa mtu mwenye maambukizi endapo utakuwa na jeraha.
  • Kuacha ngono zembe;
  • Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu ambaye hajaathirika;
  • Matumizi sahihi ya kinga (kondomu za kiume/kike);
  • Kuacha ulevi na kutumia madawa ya kulevya;
  • Kuepuka kushirikiana miswaki, nyembe, vifaa vya kutogea masikio na pua na vifaa vya kutahiri.
  • Kupungua au kupotea kwa kiasi kikubwa nguvu kazi na kuathiri utendaji wa kazi katika Utumishi wa Umma;
  • Unyanyapaa na kutengwa na jamii;
  • Kuongozeka kwa familia tegemezi.

0.6.2    Njia Zinazoweza Kutumika Kupunguza Maambukizi ya UKIMWI

  • Kuacha ngono zembe;
  • Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu ambaye hajaathirika;
  • Matumizi sahihi ya kinga (kondomu za kiume/kike);
  • Kuacha ulevi na kutumia madawa ya kulevya;
  • Kuepuka kushirikiana miswaki, nyembe, vifaa vya kutogea masikio na pua na vifaa vya kutahiri.

0.6.3    Athari za Janga la UKIMWI

  • Kupungua au kupotea kwa kiasi kikubwa nguvu kazi na kuathiri utendaji wa kazi katika Utumishi wa Umma;
  • Unyanyapaa na kutengwa na jamii;
  • Kuongozeka kwa familia tegemezi.

0.6.4    Huduma Zitolewazo kwa Mtumishi wa Umma Anayeishi na VVU

Waraka wa Utumishi wa Umma Na. 2 wa mwaka 2006 umeainisha aina mbalimbali za huduma ambazo Mtumishi wa Umma anastahili endapo atakuwa amejitambulisha kwa mwajiri kuwa anaishi na VVU. Huduma hizo ni kama zifutazo: -

  • Kupima na ushauri

Huduma ya kupima na ushauri ni haki ya kila mtumishi na inatolewe bure katika hospitali zilizochaguliwa na mwajiri.

  • Dawa

Serikali imeweka utaratibu ambapo mtumishi anayeishi na VVU atapatiwa dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo. Huduma hii inatolewa bure katika hospitali zilizochaguliwa na mwajiri

  • Chakula

Huduma ya chakula inatolewa kwa Mtumishi wa Umma aliyejitambulisha kwa mwajiri baada ya kupima na kuthibitika kuwa anaishi na VVU.

  • Usafiri

Mwajiri atagharimia usafiri na posho kwa mtumishi anayesafiri kwenda hospitali kupata matibabu ya magonjwa nyemelezi, kupima kiwango cha CD4 na kupata dawa za kurefusha maisha (ARV) kwa taratibu zilizowekwa na serikali.

Angalizo


Mtumishi aliyejitokeza na kujitambulisha kuwa anaishi na virusi vya UKIMWI ana haki ya kuomba kupangiwa kazi nyepesi na mwajiri wake ili aendelee kutoa huduma katika sehemu za kazi.

 

0.7   Umuhimu wa Kuzingatia Uwiano wa Kazi na Maisha

Kwa muda mrefu watumishi wa umma wamekumbwa na tatizo la kushindwa kuweka uwiano wa kazi na maisha yao binafsi. Hii inatokana na ukweli kwamba mtumishi wa umma anapaswa kutekeleza majukumu ya Mwajiri kwa ufanisi mkubwa huku akihitajika kisheria kufanya kazi hata baada ya muda wa saa za kazi na wakati mwingine siku za jumamosi, jumapili na siku za sikukuu. [Rejea Kanuni F. 1(2) ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009].

Ugumu wa kuweka uwiano wa kazi na maisha umesababisha baadhi ya watumishi wa umma kutokuwa na mapumziko ya kutosha na hivyo kuathiri afya zao. Baadhi ya watumishi wanashindwa kwenda likizo yao ya mwaka kwa msingi wa hofu ya kukuta mlundikano mkubwa wa kazi watakaporejea kutoka likizo. Kadhalika kitendo cha kushindwa kuweka uwiano wa kazi na maisha binafsi kimesababisha watumishi wengi kupata magonjwa yasiyoambukiza kama shinikizo la damu, kiharusi, na ugonjwa wa moyo na hivyo kuathiri utendaji wao wa kazi.

Ni kutokana na changamoto hizo, unashauriwa kutenga muda wa kufanya mazoezi, kufanya mambo yako binafsi ikiwa ni pamoja na mambo ya kukuongezea kipato kama vile biashara, kilimo na ufugaji. Ikumbukwe pia kuwa, maisha bora yanategemea matumizi mazuri ya mshahara wako pamoja na uwekezaji a utakofanya ili kujiongezea kipato.

0.8   Fursa Zilizopo Kwenye Maeneo ya Kazi

Unapaswa kubaini na kuzitumia ipasavyo fursa zilizopo kwenye eneo lako la kazi ili kuboresha maisha yako. Fursa hizo zinaweza kuwa za kiuchumi, kitalii, kijamii, kimazingira, kisanaa na kiutamaduni. Picha hapa chini inaonesha moja ya fursa ambayo ikitumika vizuri itaweza kukuongezea kipato.

0.9  TEHAMA

TEHAMA ni ufupisho wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ambayo inahusisha matumizi ya kompyuta, simu, na vifaa vingine vya kidijitali katika kufanyiza, kupata, kutuma, na kuhifadhi, taarifa na mawasiliano ili kurahisisha na kuboresha utendaji kazi, ujifunzaji na uburudikaji.

Utumiaji wa TEHAMA hutofautiana kulingana na mahitaji ambapo kuna mahitaji ya ujumla na mahitaji maalumu. Mahitaji ya jumla ni yale ambayo unapaswa kuyafahamu katika utendaji wako wa kazi wa kila siku kama vile programu mbalimbali za kompyuta mfano programu za “Word Processing”, “Excel”, “PowerPoint” na “Internet”.

Matumizi maalumu ni yale yanayohusu program maalum ambazo zinafanywa na mshiriki mwenye utaalamu maalum kama vile mifumo ya afya, rasilimali watu, fedha n.k. Sekta ya TEHAMA ni moja ya sekta zinazokua kwa kasi sana kiasi cha kuwepo matumizi makubwa ya simu za kiganjani ili kurahisha utendaji wa kazi na ujifunzaji. Pia, imerahisisha upatikanaji wa taarifa za kiutendaji na ujifunzaji kwa urahisi hali kadhalika kupata mrejesho kupitia program za simu.



0.9.1   Hali ya Matumizi ya TEHAMA katika Utumishi wa Umma

Maendeleo ya TEHAMA yamebadilisha namna ya uendeshaji wa serikali. Katika kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi serikali imewekeza katika kuboresha miundombinu, kusimika na kusambaza mifumo mbalimbali ya TEHAMA.

Mwaka 2012 serikali ilianzisha Wakala ya Serikali Mtandao na kuipa jukumu la kusimamia matumizi ya TEHAMA Serikalini. Wakala ya Serikali Mtandao ni taasisi ya Serikali yenye jukumu na mamlaka ya kuratibu, kusimamia na kukuza jitihada za Serikali Mtandao katika utumishi wa umma katika serikali kuu na MSM.

Matumizi ya TEHAMA katika taasisi za serikali yameendelea kukua kwa kasi na kuratibiwa na vitengo vya TEHAMA katika Wizara, Idara na Wakala zake lakini vilevile katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kufuatia maamuzi ya serikali ya kuwa na vitengo hivyo kwenye kila taasisi.

Tayari mageuzi ya matumizi ya TEHAMA yanaendelea kutoa matokeo chanya katika maeneo na sekta mbalimbali ambapo mifumo ya TEHAMA inatumika. Kwa sasa Serikali inazidi kupanua na kueneza mifumo hiyo katika sekta na ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya Taifa mpaka ngazi ya vituo vya kutolea huduma.

Hivyo, kama mtumishi una wajibu wa kufahamu aina ya mifumo inayotumika katika sekta au ngazi uliyopo, na kujifunza matumizi yake na salama ya mifumo hiyo. Zipo sheria na miongozo mbalimbal ya matumizi ya TEHAMA ili kuhakikisha kuwa mifumo hiyo inatumika kwa malengo mahsusi na si vinginevyo.

Serikali ilitengeneza Sera ya Taifa ya TEHAMA (2016) ikiwa na dira ya kuifanya Tanzania kuwa na jamii yenye ufahamu wa kutosha wa matumizi TEHAMA kwa maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

0.9.2   Umuhimu wa Matumizi ya TEHAMA katika Utumishi wa Umma

TEHAMA imeleta tija kubwa katika utendaji wa shughuli mbalimbali mahali pa kazi.

  •  Kuchakata taarifa kwa ufanisi 

Urahisi wa kuchakata taarifa kwa muda mfupi na kurahisisha urejeaji wa taarifa zinapohitajika. 


  • Kuhifadhi taarifa na nyaraka mbalimbali 

Uhifadhi wa taarifa mbalimbali huondoa mlundikano wa mafaili na hivyo kutatua changamoto ya uhaba wa vyumba vya kuhifadhia mafaili na nyaraka mbalimbali.

  • Kuhudumia wateja wengi kwa muda mfupi

TEHAMA inarahisha taarifa kuwafikia wateja wengi kwa muda mfupi hivyo kuokoa muda ambao ungepotea kwa kupanga foleni, na hivyo kuruhusu kufanyika mambo mengine ya uzalishaji. Vile vile TEHAMA huwezesha uwasilishaji wa nyaraka na taarifa mbalimbali baina ya watumishi na wasimamizi hivyo kuharakisha utoaji wa maamuzi kwa haraka zaidi.

  • Kurahishisha ufundishaji na ujifunzaji

TEHAMA imewezesha ufundishaji na ujifunzaji kwa njia za kielektroniki kwa ufanisi zaidi hivyo kuokoa muda na pesa nyingi ambazo zingetumika endapo mafunzo yangefanyika ana kwa ana.

  • Uhifadhi wa mazingira 

Matumizi ya TEHAMA katika utendaji wa kazi za kila siku inasaidia kupunguza matumizi ya karatasi katika kuandaa na kusambaza taarifa hivyo kupuunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na kukata miti kwa ajili ya kutengeneza karatasi.

  • Kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato

Serikali imefanya juhudi mbalimbali za kuboresha ukusanyaji wa mapato nchini kupitia mifumo ya TEHAMA. Kwa mfano, matumizi ya Mfumo wa Ukusanyaji wa Mapato katika MSM

 

0.9.3    Sheria na Miongozo ya Matumizi ya TEHAMA

Pamoja na faida na umuhimu wa kutumia TEHAMA ili kuboresha utendaji kazi, yawezekana yakawepo matokeo hasi endapo TEHAMA itatumika vibaya. Ili kuhakikisha TEHAMA inaleta tija katika utendaji wa kazi na ili kuepukana na matokeo hasi serikali iliandaa sheria na miongozo mbalimbali kuhakikisha matumizi sahihi ya vifaa na mifumo ya TEHAMA. Mwongozo wa Matumizi Bora, Sahihi, na Salama ya Vifaa na Mifumo ya TEHAMA Serikalini (2012) umeainisha masuala muhimu ambayo yanapaswa kuzingatiwa.

0.9.4    Matumizi ya Anwani za Barua Pepe

Unapaswa kutumia barua pepe za serikali kutuma au kupokea nyaraka za serikali. Aidha barua pepe za serikali ni kwa matumizi ya shughuli za serikali tu na si vinginevyo. Mwongozo wa Matumizi Bora, Sahihi, na Salama ya Vifaa na Mifumo ya TEHAMA Serikalini (2012) umetoa tahadhari zifuatazo

  • Kuwa makini wakati wa kutuma barua pepe za jumla zenye kuruhusu watu wengi kupokea ujumbe kwa wakati mmoja ili kuepuka kutuma ujumbe kwenda kwenye anuani isiyokuwa ya Taasisi ya Serikali.
  • Usitume barua na nyaraka siri kupitia mfumo wa barua pepe.
  • Ni kosa kutumia anwani ya barua pepe ya Serikali kujisajili katika mitandao ya jamii, kama vile “Face book”, “Blog za kijamii”, “Twitter” n.k.
  • Haushauriwi kutumia kompyuta nje ya Ofisi za Serikali kama vile “Internet Café” kupokea au kutuma taarifa za Serikali.

Kisa Mkasa 


Bi Rose Mkubwa ni Mkuu wa Idara ya Habari. Muda wa jioni akiwa katika sherehe ya harusi ya binti yake alipokea simu kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri akimwagiza kutuma nyaraka ya siri yenye taarifa muhimu za watumishi ambao wanapaswa kupunguzwa kazini kutokana na sababu mbalimbali na ni suala la dharura. Kwa kuwa taarifa imemfikia kwa dharura alitakiwa arudi nyumbani ambako kuna kompyuta mpakato ya ofisini yenye nyaraka. Hata hivyo, akiwa katika sintofahamu alikumbuka kuwa amewahi kujitumia kwenye barua pepe yake ya “gmail” kama chelezo (backup) hivyo aliamua kuituma nyaraka hiyo kwa kutumia simu yake ya kiganjani.
Baada ya kutuma akiwa anarudi ukumbini kwa bahati mbaya vibaka wanakwapua ile simu yake na kutokomea kusikojulikana. Kesho yake taarifa zinazohusu nyaraka hizo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii na hivyo kuzua taharuki katika jamii. Uchunguzi unaonesha kwamba chanzo cha kuvuja kwa taarifa ile ni simu ya Bi. Rose iliyokwapuliwa.
Maswali
  1. Kwa kuzingatia maelezo na kisa hiki bainisha makosa yaliyofanywa na Bi Rose.
  2. Unadhani Bi Rose alipaswa kufanya nini ili kuepusha makosa aliyofanya?

 

8.9.5    Mfano wa Makosa na Adhabu za Matumizi ya TEHAMA

   i).        Kuingia kwenye kompyuta bila idhini

Huruhusiwi kutumia au kuruhusu kompyuta kutumika kinyume cha sheria kwa makusudi, kwani kosa hili linaweza kusababisha adhabu ya faini au kifungo au vyote kwa pamoja kwa mujibu wa sheria [Rejea kifungu Na 4(1) cha Sheria ya Makosa ya Mtandao (2015)]

  ii).        Matumizi ya mfumo wa kompyuta baada ya muda wa idhini ya kutumia kuisha

Huruhusiwi kuendelea kutumia mfumo wa kompyuta kinyume cha sheria kwa makusudi baada ya kumalizika muda ulioruhusiwa kutumia mfumo huo kama vile kukoma utumishi wako, kubadilishwa cheo n.k. [Rejea kifungu Na 5(1) cha Sheria ya Makosa ya Mtandao (2015)].

 iii).        Matusi ya kibaguzi

Huruhusiwi kumtukana au kumfedhehesha mtu mwingine kupitia mfumo wa kompyuta, kwa kigezo cha moja kati ya kundi linalotambulika kwa tabaka, rangi, asili, utaifa, kabila au dini fulani (Rejea kifungu Na 18 (1) cha Sheria ya Makosa ya Mtandao (2015)).

 iv).        Mauaji ya kimbari na makosa dhidi ya ubinadamu 

Huruhusiwi kuchapisha au kusababisha kuchapishwa kinyume na sheria mambo yanayochochea, kukanusha, kupunguza au kuhalalisha matendo yanayoweza kusababisha mauaji ya kimbari au makosa dhidi ya ubinadamu kwa kupitia mfumo wa kompyuta. [Rejea kifungu Na 19 (1) cha Sheria ya Makosa ya Mtandao (2015)].

Angalizo


Makosa na adhabu zilizoainishwa katika mada hii ni baadhi tu, yapo makosa na adhabu zingine ambazo unapaswa kuzingatia. [Rejea Sheria ya Makosa ya Mtandao, 2015 na Mwongozo wa Matumizi Bora, Sahihi, na Salama ya Vifaa na Mifumo ya TEHAMA Serikalini (2012)]

 






Matangazo

  • Wanafunzi waliochaguliwa Shule za Vipaji maalumu,Ufundi,Bweni kawaida na shule maalumu 2023 December 14, 2022
  • wavulana waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2023 simanjiro day schools December 14, 2022
  • wasichana waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2023 Wilaya ya Simanjiro day schools December 14, 2022
  • Tangazo la Ajira Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro May 23, 2022
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • Nyerere day

    October 14, 2024
  • Mkutano wa wadau kuhusu utoaji wa maoni ya Dira ya Maendeleo ya mwaka 2050

    July 29, 2024
  • MWENGE WA UHURU

    July 16, 2024
  • Kifo Cha Raisi awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi 2024

    February 29, 2024
  • Ona vyote

Video

Mh.Dr Serera azindua kipindi cha Pili awamu ya Tatu ya TASAF Wilayani Simanjiro
video Zaidi

Fika kwa Haraka

  • Government Mailing System
  • Mission and Vision
  • Organization Structure
  • Completed Projects

Kiungo Muunganisho

  • Ikulu
  • Utumishi
  • Matokeo kidato cha sita 2021
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Idara ya Habari-Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Government Mailing System

copyright@2016 Halmashauri ya Wilaya Simanjiro.Haki zote zimehifadhiwa