SHUGHULI ZA UVUVI WILAYANI SIMANJIRO
Halmashauri ya Wilaya Simanjiro ni Halmashauri mojawapo kati ya halmashauri zinazojishughulisha na shughuli za uvuvi.
Shughuli hizi za uvuvi zinafanyika zaidi katika Bwawa la nyumba ya mungu ambapo bwawa hili linatumika katika shughuli hizi
kwa mikoa ya Manyara na Kilimanjaro.shughuli hizi za uvuvi katika wilaya ya simanjiro kwa kushirikiana na mkoa wa kilimanjaro,
hufanyika kwa msimu kwani kila baada ya miezi sita bwawa hili hufungwa ili kupisha samaki waweze kuzaliana na kukua
ikiwa na madhumuni ya kuendeleza kizazi cha samaki hao.
Aidha katika shughuli hizi pia zinafanyika katika Bwawa la kidawashi lililoko karibu na mji mdogo wa mirerani.Pia katika bwawa hili
shughuli hizi hufanyika kwa kipindi cha mwaka mzima na halmashauri huingiza mapato ya ndani mengi kupitia chanzo hiki.
copyright@2016 Halmashauri ya Wilaya Simanjiro.Haki zote zimehifadhiwa