• Email za Serikali |
    • Malalamiko |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Mawasiliano |
    • Mifumo |
Simanjiro District Council
Simanjiro District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro

  • Mwanzo
  • About us
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Administration
    • Muundo wa Halmashauri
    • Sehemu
      • Infastructure,Rural and Urban Development
        • Works
        • Roads
        • Rural & Urban Development
      • Health,Social Walfare & Nutrition Services
        • Health Services
        • Nutrition Services
        • Social Walfare
      • Industry ,Trade and Investment
        • Industry Development & Investment
        • Trade & Marketing
      • Pre-Primary & PPrimary Education
        • Academics
        • Special Needs Education
        • Adult & Non Formal Education
      • Seconadry Education
        • Academics
        • Statistics & Logistics
        • Special Needs
        • Adult & Non Formal Education
      • Community Development
        • Cross-Cutting Issues Cordination
        • Ngos's & Cbos's Coordination
      • Agriculture,Livestock and Fisheries
        • Agriculture
        • Livestock
        • Fisheries
      • Administration & Human Resources Management
        • Human Resource Management
        • Utawala
      • Planning and Coordination
        • Planning and Budgeting
        • Monitoring and Evaluation
      • LGA'S LAND ADMINISTRATION OFFICE-Ministry of Land ,Housing and Humman Settlement
    • Vitengo
      • Sports,Culture & Arts
      • ICT Unit
      • Government Communication Unit
      • Waste Management & Sanitation Unit
      • Legal Services Unit
      • Internal Audit Unit
      • Procurement Management Unit
      • Natural Resources & Environment Unit
      • Finance & Accounts Unit
  • Fursa za Uwekezaji
    • Madini
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Utoaji wa Leseni za Biashara
    • Utoaji wa Lesseni za Vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa Leseni Za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya Asilimia Kumi(10%)
    • Upimaji wa Ardhi
    • Usajili wa Vikundi vya Kijamii
    • Uandikishaji wa Bima ya Afya ya Jamii(iCHF)
    • Utoaji wa Vitambulisho vya Wajasiriamali Wadogo
    • Kulipia Tozo Za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Huduma za Halmashauri
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
    • Suku ya Kumwona Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Report
    • Vipeperushi
    • Miongozo Mbalimbali
    • By Laws
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Hotuba

Kikao cha Dcc Wilayani Simanjiro

Imetumwa lini: December 2nd, 2021

Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mh. Dr Suleiman Serera alifungua na Kuendesha kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro tarehe 2/12/2021 ambapo wajumbe mbalimbali kutoka katika taasisi za dini ,taasisi binafsi  pamoja na taasisi za serikali walihudhuria .

Katika kikao hicho taarifa kutoka katika idara mbalimbali za halmashauri pamoja na taasisi za serikali zilizopo katika Wilaya ya Simanjiro ziliwasilishwa .

Katika Idara ya Ardhi na Maliasili  Wajumbe walimpongeza Mkuu wa Idara hiyo Bw. Baltazari Sule kwa kushughulikia  na kupunguza migogoro ya Ardhi katika Wilaya ya Simanjiro ,Pia wajumbe wa kikao hicho  waliishauri idara hiyo kuhamasisha wananchi kupanda miti ya matunda,kutokuvuna miti ya asili pindi wanapoandaa mashamba kwa ajili ya kilimo,kuongeza doria katika barabara ya Komolo, Oljoro No. 5 na Losinyai ili kupunguza  wahalifu wanatumia pikipiki kusafirisha mkaa.Pia Idara hiyo ilishauriwa kufanya doria mara kwa mara ili  kudhibiti uharibifu wa mazingira.wajumbe waliendelea kwa kuishauri Idara hiyo kulinda maeneo ya hifadhi na njia za Ikolojia ya wanyama ya Langai-Ngage , Pia idara ilitakiwa kudhibiti  Biashara ya nyama pori zinazosafirishwa kwenda  Wilaya ya Kilindi hivyo Suala la ujangili lishughulikiwe kwa  kushirikiana na vijiji husika

Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mh.Christopher Ole Sendeka  alitoa pongezi kwa Idara hiyo na Shirika la UCRT kwa kushughuliki migogoro ya Ardhi Wilayani Simanjiro na kupanga matumizi bora ya Ardhi.Pia alishauri kuwa maeneo yanayokuwa kama Terrat, Nyumba ya Mungu, Naberera, Langai na maeneo yanayopakana na Endonyongijape yawekewe  utaratibu wa kupima na kupangwa.

Wajumbe waliendelea kushauri kuwa Idara ya Ardhi ichukue hatua  kwa wale waliojenga bila vibali vya ujenzi kutoka Halmashauri, Pia walishauri kuwa  eneo la Mji  Mdogo wa Orkesumet liendelee kupimwa na kutengwa maeneo kama ramani inavyoonesha,Eneo la Ikulu lipimwe vizuri na kuwekewa uzio kwa ajili ya ulinzi, watu wasiruhusiwe kujenga maeneo yaliyo karibu na  visima vya maji wala kuelekea eneo la milima.Pia walishauri kuwa eneo la Kijiji cha Losinyai lipimwe  ili Halmashauri iweze kuandaa taratibu za uuzaji wa viwanja kwa ajili ya makazi na biashara katika kijiji hicho .


Viongozi wa dini  nao walikumbusha kuwa Maeneo yanapopimwa kubainishwe maeneo ya Ibada, taasisi, mapario ya mifugo na maeneo ya visima vya maji  ili kuondoa malalamiko na muingiliano itakayosababisha migogoro ya Ardhi.

Katika Idara ya Maendeleo ya Jamii wajumbe walimpongeza Mkuu wa Idara hiyo Bi.Asia Ngalisoni kwa kupanua wigo wa utoaji mikopo kwa vikundi vya vijana wanawake na watu wenye ulemavu.

Mh.Mkuu wa Wilaya pamoja na Mh.Mbunge wa jimbo la Simanjiro walisisitiza Idara hiyo kutoa elimu ya Hedhi salama kwa wazazi.

Pia Mwenyekiti wa  Halmashauri Mh.Baraka Kanunga Laizer alimshauri Mkuu wa Idara ya Maendeo ya Jamii awasiliane na Ofisi ya RED CROSS  katika kutoa Elimu ya Hedhi na ugawaji wa taulo za kike na jinsi ya kushona taulo za kike kwa kutumia kitambaa na uzi ili kupunguza gharama za ununuaji wa taulo hizo kwa wazazi wasio na uwezo mkubwa wa kifedha. Pia wajumbe waliishauri idara hiyo kutoa  Mafunzo ya Hedhi na ugawaji Taulo za Kike kwa wanafunzi wa Shule zote  za sekondari zilizopo katika Wilaya ya Simanjiro.

Katika Idara ya Elimu Msingi Afisa Elimu Msingi Bw.Silvanus Tairo aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kwa kipindi cha Januari – Novemba, 2021 ikianisha Utekelezaji  wa shughuli za Idara, Sababu za kutofikia malengo ya ufaulu, Mikakati ya muda mfupi

Wajumbe waliishauri idara hiyo kutambua michango ya wadau wa elimu na  michango/taarifa zao ziwe zinawasilishwa katika vikao mbalimbali vya kiserikali. Aidha Katika kikao hicho Mjumbe alihoji kuhusu uhalisia wa bei ya vyakula kwa shule za msingi za bweni na sekondari kwani  haziendani na bei halisi ya soko kulingana na taarifa iliyotolewa.Pia wajumbe walimshauri Mkurugenzi Mtendaji wa Hamashauri  ya Wilaya ya Simanjiro kutenga fedha kwa ajili ya ukarabati wa shule chakavu Orkesumet, Naberera na nyinginezo.

Mkuu wa Wilaya  Mh. Dr Suleiman Serera alimuagiza Afisa Elimu Msingi kuandaa taarifa sahihi ya takwimu za wanafunzi wanaonza na kumaliza darasa la saba kuingia sekondari na  kufanya tathimini ya ufaulu katika ngazi ya Kitaifa na Kimkoa na taarifa hiyo  iwe  inajadiliwa katika vikao vya mbalimbali vya Wadau wa Elimu,Pia aliagiza kuwa  Mkurugenzi Mtendaji afanye ukaguzi maalum (Special Audit) kwa shule za Msingi za bweni na shule za sekondari ili kuona mlinganisho wa bei wanayonunulia chakula na bei iliyoko sokoni na kubaini matumizi sahihi ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya ununuzi wa vyakula katika shule hizo,Pia alishauri Viongozi wa ngazi zote wafanye uhamasishaji wa upatikanaji  na utoaji wa chakula cha mchana mashuleni,Pia aliwataka Viongozi wote haswa wa ngazi ya Kata wachukue hatua kudhibiti  utoro kwa  kufuatilia na kukagua mahudhurio ya wanafunzi na walimu na kuhakikisha wanafunzi hao wote wanahitimu masomo yao,Aidha alimtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro kuitisha  kikao cha Wadau wa Elimu ili kuweka mikakati thabiti ya kuinua kiwango cha  elimu katika Wilaya ya Simanjiro.

Katika Idara ya Afya Mh. Mkuu wa Wilaya aliagiza kuwa vituo vya afya na Zahanati kuwa na taarifa sahihi za dawa na vifaa tiba ,matumizi ya Mifumo ya Hospitali(Got-Homis ,Ichf pamoja  NHIF )katika utoaji wa huduma na utunzaji wa taarifa mbalimbali zikiwemo za mapato yanayotokana na utoaji wa huduma na uuzaji wa dawa mbalimbali katika vituo vya afya na zahanati hizo .

Pia   wajumbe walishauri kupanuliwa na kuongezwa wodi za wagonjwa katika kituo cha Afya Mirerani ili kuhimili ongezeko la wagonjwa katika kituo hicho.Pia walishauri idara ya Afya kupanga Mikakati maalumu na ya Haraka ya kudhibiti ongezeko kubwa la maambukizi ya Virusi vya Ukumwi(VVU) katika mji mdogo wa Mirerani ,Pia walishauri vyombo vya ulinzi na uslama kudhibiti biashara ya Madanguro katika mji wa mirerani ili kupunguza kasi ya Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi katika mji huo.Aidha Wajumbe walilalamikia lugha mbaya kwa watoa huduma katika vituo vya Afya vya Serikali  haswa Mirerani na Orkesumet hivyo wateja wengi kuamua kwenda katika vituo vya Afya na Zahanati zinazomilikiwa na taasisi na watu binafsi ili kupata huduma hizo.

Katika Idara ya Mifugo na Uvuvi wajumbe walishauri kuwa Idara hiyo kutafuta mbinu mbadala za kuwasaidia wafugaji kupata chaku;la cha mifugo wakati wa kipindi hiki cha ukame,Pia walishauri idara hiyo kufanya tafiti kabla ya kuleta chanjo mbalimbali za magonjwa ya mifugo ili kuepusha mifugo kudhurika na chanjo zisizofaa.Pia wajumbe walishauri idara hiyo kutoa elimu kwa wafugaji  ya kuandaa malisho mbadala ya mifugo ili yaweze kutumika kipindi cha ukame.

Katika taasisi ya Ruwasa pamoja   mamlaka ya maji na usafi wa mazingira orkesumet (ouwasa) wajumbe walishauri  kuwafungia  miundombinu ya huduma ya maji wateja waliokamilisha taratibu za kupatiwa huduma hiyo  . Pia walizishauri taasisi hizo kuweka  utaratibu mzuri wa kupandisha maji ya kutosha na kujaza matenki ili kuwa na maji ya kutosha muda wote.

KatikaTaasisi ya TARURA wajumbe waliishauri taasisi hiyo kujenga miundombinu mizuri ya kupitisha maji ( Calvat)  itakayomudu kiasi cha maji katika kipindi cha mvua kubwa,Wajumbe  walitoa mfano wa  Barabara za Msitu wa Tembo, Ngorika, Shambarai-Arumeru zinazozidiwa na maji wakati wa kipindi cha mvua  kubwa. Pia walishauri kuwa Barabara zinazotengenezwa ziwekwe changarawe badala ya udongo unaoleta vumbi na pia kuwepo  vibao  na alama za barabarani  zinazoonyesha maeneo hatarishi na maeneo ya vivuko vya Mifugo.

Viongozi wa Wilaya waliiagiza TARURA kuwashirikisha  viongozi wa maeneo husika pindi wanapojenga miradi ya barabara.

Katika taasisi ya tanesco wajumbe waliishauri taasisi hiyo kuharakisha  upatikanaji wa nguzo za umeme na kuwapatia wateja ambao wamekidhi vigezo vya kufungiwa umeme.

Katika Taasisi ya NIDA wajumbe waliishauri taasisi  hiyo kuendelea kufuatilia upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa kwa wakati.

Katika Taasisi ya Kuzuia na Kupamabana na Rushwa TAKUKURU wajumbe waliishauri taasisi hiyo  kuendelea kuimarisha klabu za Rushwa mashuleni na kutoa elimu ya Rushwa kwa jamii ili kupunguza vitendo vya upokeaji na utoaji wa rushwa maofisini na katika jamii.

 Taasisi ya  Polisi  ilishauriwa kutoa mrejesho wa taarifa ya  Mashirika yanayofuatilia na kutetea ukatili na Unyanyasaji wa Kijinsia ili wananchi waelewe mwenendo wa kesi hizo.Pia wajumbe walishauri Jeshi la Polisi lisimamie ratiba ya kuondoka kwa Mabasi ya asubuhi Mjini Orkesumet – Arusha pamoja na mabasi yanayotoka Arusha kuelekea Wilayani   Kiteto ili kuthibiti ajali zinazotokana na mwendo wa kasi wa mabasi hayo.

Katika mada zinginezo Mh ,Mkuu wa wilaya alikiagiza chama cha walimu(CWT)  Wilayani Simanjiro kiifuatilie upatikanaji wa walimu ili kupunguza uhaba wa waalimu katika shule za Msingi na Sekondari Wilayani Simanjiro.

Mwisho Mkuu wa Wilaya Mh. Dr.Suleiman Serera aliwapongeza na kuwashukuru  wadau wa elimu pamoja na Wadau wa maendeleo  wote  waliochangia katika Miradi na shughuli mbalimbali za serikali Wilayani Simanjiro ,Pia aliwapongeza Viongozi na wataalamu wote wa Wilaya kwa kazi nzuri wanazozifanya  katika kutekeleza majukumu ya kiserikali na kuwaagiza kutekeleza  kwa wakati maagizo yote yaliyotolewa katika kikao hicho.

Matangazo

  • Wanafunzi waliochaguliwa Shule za Vipaji maalumu,Ufundi,Bweni kawaida na shule maalumu 2023 December 14, 2022
  • wavulana waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2023 simanjiro day schools December 14, 2022
  • wasichana waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2023 Wilaya ya Simanjiro day schools December 14, 2022
  • Tangazo la Ajira Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro May 23, 2022
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • Nyerere day

    October 14, 2024
  • Mkutano wa wadau kuhusu utoaji wa maoni ya Dira ya Maendeleo ya mwaka 2050

    July 29, 2024
  • MWENGE WA UHURU

    July 16, 2024
  • Kifo Cha Raisi awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi 2024

    February 29, 2024
  • Ona vyote

Video

Mh.Dr Serera azindua kipindi cha Pili awamu ya Tatu ya TASAF Wilayani Simanjiro
video Zaidi

Fika kwa Haraka

  • Government Mailing System
  • Mission and Vision
  • Organization Structure
  • Completed Projects

Kiungo Muunganisho

  • Ikulu
  • Utumishi
  • Matokeo kidato cha sita 2021
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Idara ya Habari-Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Government Mailing System

copyright@2016 Halmashauri ya Wilaya Simanjiro.Haki zote zimehifadhiwa