HALI YA VIWANDA WILAYANI SIMANJIRO.
Wilaya ya simanjiro ina jumla ya viwanda 421 vidogo, vya kati na vikubwa. Viwanda vinanyofanya kazi ni 415 na thamani ya viwanda hiyo inakadiriwa kuwa ni Tsh.4,921,900,000.00 ikiwa na jumla ya wafanyakazi 1,922. Aidha kwa sasa Wilaya ina jumla ya viwanda vipya vitano (5) ambavyo vipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji vyenye thamani ya jumla ya Tsh.4,092,600,000 na vitaweza kuajiri wafanyakazi wapatao 313 kama jedwali linavyonyesha hapa chini.
Jedwali namba 6. Orodha ya viwanda vipya Simanjiro
Kiwanda |
Kadirio la Mtaji |
Kadirio la Watumishi |
Hali ilivyo sasa |
Kiwanda cha Unga na Chakula cha Mifugo –Orkesumet
|
40,000,000.00
|
8 | Kinatarajia kuanza Mwishoni mwa mwaka 2021 |
Kiwanda cha Mikate – Mirerani
|
50,000,000
|
8
|
Kinatarajia kuanza mwishoni
mwa amwaka 2021 |
Graphite Platimun –Naisinyai
|
1,500,000,000
|
150
|
Kiwanda kinaendelea na Shughuli zake |
God Mwanga Gem – Endiamutu
|
2,500,000,000
|
150
|
Kiwanda kinafanya uzalishaji |
Mashine ya Kusaga Nafaka Mirerani
|
2,600,000.
|
2
|
viwanda hivyo vinafanya kazi |
JUMLA
|
4,092,600,000
|
318
|
|
5.1 Mikakati ya kujenga viwanda vipya na kufufua viwanda vilivyokufa
Halmashauri imeweka mikakati ya kujenga na kufufua viwanda kumi na tano (15). Aidha, Wilaya imeunda kamati ya kuhamasisha ujenzi wa viwanda vipya na ufufuaji wa viwanda vilivyokufa. Mikakati hiyo ni pamoja na;
Kila kijiji kimeagizwa kutenga ekari ishirini (20) kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda ambapo hadiilipofika Aprili 2018 vijiji kumi na tatu (13) vimeshatenga maeneo hayo sawa na ekari 260. Vijiji hivyo ni Lemkuna, Loiborsoit B, Gunge, Msitu wa Tembo Mji wa Orkesumet, Londoto, Einoti, Engonongoi, Komolo, Nadonjukin, Losinyai, Oljoro No.5 na Kimotorock.
Halmashauri kupima maeneo hayo, kuyaandalia hatimiliki na kuhamasisha wananchi kuyatumia kwa ajili ya viwanda kwa ubia na wawekezaji wa maeneo yao.
Eneo lenye ukubwa wa ekari 35 limetengwa katika mji mdogo wa Orkesmet kwa ajili ya viwanda mchanganyiko
Kualika wadau wa maendeleo kutoka sekta binafsi ili washiriki katika utekelezaji wa mikakati ambayo wilaya imeweka. Kikao cha kwanza cha wadau kilifanyika tarehe 10.3.2018 na wadau mbalimbali wameonesha nia ya kuwekeza kwenye maeneo ya viwanda vya kusindika nafaka wakiratibiwa na TCCIA wilaya ya Simanjiro.
Kuunda Task force inayoongozwa na Mkuu wa wilaya kufanya vikao vya mara kwa mara (kila wiki) ili kuweka mikakati mipya na kutathmini mikakati iliyowekwa na kuiboresha.
Viwanda vilivyokuwepo ambavyo vimekufa au vimeacha kuzalisha vifuatiliwe na task force ili kuona uwezekano wa wadau wengine kuvifufua na kuviendeleza. Mfano mzuri ni viwanda vilivyokuwa katika eneo la Rotiana Naberera. Viwanda hivi (Nyama, maziwa, asali, Mkaa) vinaweza kufufuliwa kwa jitihada za pamoja kati ya Serikali na wadau wa maendeleo wenye nia ya kuendeleza viwanda hivyo.
Kufanya uhamasishaji kupitia mikutano ya wananchi na vyombo vya habari kutangaza fursa za uwekezaji wa viwanda zilizopo. Tayari Mkuu wa Wilaya amepata fursa ya kutangaza masuala ya viwanda kwenye radio Terrat, Kili FM pamoja na kufanya mahojiano na vyombo mbalimbali kama ITV, Channel Ten na TBC kuhusu fursa hizo wilayani. Kauli mbiu inayotumika ni “Simanjiro yetu viwanda vyetu”.
Halmashauri ya Wilaya Simanjiro Bomani street-Orkesumet
Sanduku la Posta: P.o Box 9596,Orkesumet,Simanjiro,Manyara,Tanzania
Simu: Tel:027-29707889
Simu: +255-758350936
Barua pepe: ded@simanjirodc.go.tz
copyright@2016 Halmashauri ya Wilaya Simanjiro.Haki zote zimehifadhiwa