KITENGO CHA UKAGUZI WA NDANI (INTERNAL AUDIT UNIT)
Utangulizi
Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani ni kitengo ambacho kina jukumu la kutoa ushauri ili kusaidia idara nyingine ndani ya Halmashauri kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Madhumuni ya kitengo
Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani kina wajibu wakufanya kaguzi juu ya utekelezaji wa majukumu ya Halmashauri pamoja na usimamizi wa rasilimali za Halmashauri na kutoa ushauri kwa afisa masuuli unaolenga kuboresha huduma za Halmashauri pamoja taratibu sahihi na zinazokubalika za usimamizi wa masuala ya fedha ili kufikia malengo yaliyopangwa.
Muundo wa kitengo
Kitengo cha ukaguzi wa ndani kinaongozwa na Mkaguzi mkuu wa Ndani ambaye anawajibika kwa Afisa masuuli akisaidiwa na Wakaguzi wa Ndani.
Majukumu ya kitengo cha Ukaguzi wa Ndani.
Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani kina majukumu yafuatayo:-
Kupitia mifumo mbalimbali ya udhibiti (“internal control systems”) na kutoa ushauri kwa Afisa Masuuli juu ya uboreshaji wake.
Kupanga na kufanya ukaguzi kwa kuzingatia maeneo yenye vihatarishi vitakavyosababisha kutofikia malengo ya Halmashauri (High risk areas).
Kusaidia uwongozi wa Halmashauri kuboresha utendaji ili malengo yaweze kufikiwa kwa kutoa ushauri mbalimbali kama inavyohitajika .
Kupitia kanuni, sheria na taratibu mbalimbali zilizowekwa na wizara/serikali na kutoa ushauri juu ya utekelezaji wake.
Kukagua na kutoa ushauri kwa afisa masuuli juu ya matumizi, utunzaji na usimamizi wa rasilimali zote za serikali.
Kukagua utendaji/utekelezaji wa majukumu ya Halmashauri na kushauri.
Kuratibu mafunzo ya kanuni na sheria za fedha manunuzi pamoja na uthibiti wa vihatarishi.
Kazi nyingine zinazoelekezwa na afisa masuuli.
Kuandaa mpango mkakati wa Ukaguzi.
Kuratibu kazi za ukaguzi
Kufanya ukaguzi wa akaunti za vijiji, Hospitali na mashule yanayopokea fedha kutoka Halmashauri
Kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo.
Kupitia taarifa za ukaguzi wa ndani na nje kwa kushirikiana na uwongozi.
Kupitia na kutoa taarifa juu ya majibu ya menejimenti kwenye taarifa za ukaguzi wa ndani na kuisaidia menejimenti kwenye utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa kwenye taarifa mbalimbali na ufuatiliaji kwenye utekelezaji wa mapendekezo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Kupitia na kutoa taarifa juu ya uwezo/ufanisi wa udhibiti uliopo kwenye mifumo iliyounganishwa na kompyuta.
NA
|
JINA
|
CHEO
|
1
|
Menfrid N. Nyakasi
|
DIA
|
2
|
Oscar A. Pessa
|
IA
|
3
|
Lonyamali N. kivuyo
|
IA
|
Changamoto za Kitengo:
Halmashauri ya Wilaya Simanjiro Bomani street-Orkesumet
Sanduku la Posta: P.o Box 9596,Orkesumet,Simanjiro,Manyara,Tanzania
Simu: Tel:027-29707889
Simu: +255-758350936
Barua pepe: ded@simanjirodc.go.tz
copyright@2016 Halmashauri ya Wilaya Simanjiro.Haki zote zimehifadhiwa