• Wasiliana Nasi |
    • Maswali yanayoulizwa Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
Simanjiro District Council
Simanjiro District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Chimbuko/Asili
      • Ukubwa wa Eneo
      • People of Simanjiro
      • Hali ya Hewa
      • Economic Activities
      • Orodha ya Viongozi
    • Dira na Moto
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Organization Structure
    • Vitengo
      • Internal Audit
      • Law
      • Procurement and supply
      • Bees
      • Election
      • ICT
    • Idara
      • Administration and Management
      • Agriculture and Irrigation
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Primary Education
      • Secondary Education
      • Health
      • Land,Natural Resources and Environment
      • Community Development
      • Finance and Trade
      • Works and
      • Envirnment and Cleanliness
      • Water
    • Departiment/Units Activities
    • Linki ya Machapisho
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mineral Extraction
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Huduma za Halmashauri
      • Mipango na Mazingira
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
      • Vikao vya Waheshiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • By Laws
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Report
  • Kituo cha Habari
    • Notice to the Public
    • National and Office gallery
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Makataba ya Picha

Health

TAARIFA YA IDARA YA AFYA KWA AJILI YA TOVUTI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA SIMANJIRO

UTANGULIZI

Idara ya Afya ina jumla ya vituo 32 vya kutolea huduma ikiwa ni Vituo vya afya vitatu (3) na zahanati 29 za Serikali.

Vituo vya afya vipo katika Kata za Orkesumet, Naberera na Mirerani. Zahanati zipo katika vijiji vya Namalulu, Sukuro, Terrat,Narakauwo, Loiborsiret, Kimotorok, Loiborsoit A, Oljoro No.5, Kilombero, Naisinyai, Nomeut, Lengasit, Msitu wa Tembo, Magadini, Ngorika, Nyumba ya Mungu, Lemkuna, Ochoronyori, Landani, Losokonoi, Ngage, Loiborsoit B, Ruvu Remit, Gunge, Kitwai A ,Kitwai B, Engonongoi, Loborsiret na Orkesumet.

Idara ya afya ina timu  ya uendeshaji ya huduma za afya wilaya(CHMT) ambayo ina timu  mbalimbali kama timu  ya dharura(emergency team),kamati ya kupitia taarifa(technical team),timu ya kukagua matumizi ya dawa(drug auditing team)kamati ya matibabu(therapeutic committee),timu ya kuboresha huduma za afya(quality improvement team) n.k

Maandalizi ya timu ya dharura

WATUMISHI

Idara inakada mbalimbali kama ifuatavyo kwenye jedwali;


Sna
Aina ya kada

Idadi

1.
Madaktari

5

2.
MadaktariWasaidizi

6

3.
Matabibu

23

4.
Tabibu Msaidizi

1

5.
Makatibu wa Afya

2

6.
Maafisa Afya

7

7.
Muuguzi Mkuu

1

8.
MaafisaWauguziWasaidizi

30

9.
Wauguzi

47

10.
Wahudumu wa Afya

65

11.
Mfamasia

1

12.
MteknolojiaMaabara

1

13.
Wasaidizi wa Maabara

2

14.
Mteknolojia Madawa

1

15.
Mtunza Kumbukumbu

2

16.
Afisa Ustawi wa Jamii

1

17.
Wapishi

3

18.
Dobi

1


Jumla

199


 

MADHUMUNI YA IDARA YA AFYA NI KUTOA HUDUMA ZA TIBA, KINGA NA USHAURI KWA JAMII KWA KUPITIA VITENGO VYAKE.

Katika idara ya Afya kunavitengo 16

  • Kitengo cha Afya Chanjo
  • Kitengo cha dawa
  • Kitengo cha Kifua Kikuu/Ukoma
  • Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto
  • Kitengo cha Afya Mazingira
  • Kitengo cha Maabara
  • Kitengo cha Macho
  • Kitengo cha Afya ya kinywa na meno
  • Kitengo cha iCHF& CHF
  • Kitengo cha Bimaya Afya
  • Kitengo cha Ustawi wa jamii
  • Kitengo cha Ukimwi
  • Kitengo cha Huduma majumbani kwa wagonjwa
  • Kitengo cha Lishe
  • Kitengo cha kifua Kikuu na Ukimwi
  • Kitengo cha Tiba Mbadala
  • Kitengo cha Magonjwayasiyopewakipaumbele

1. Kitengo cha Afya Chanjo

Kitengohikihufanyashughulizifutazo;

  • Kufuatiliakusimamiautekelezajinamiongozo sera mbalimbali zinazotolewa na Wizara.
  • kuhakikishaupatikanaji wa chanjo na vifaa vyakemitungi yagesivituoniinakuwepo kwa mudawote kulingana na mahitaji.
  •  Kufanya matengenezomadogomadogo ya majokofu.
  • Kukusanya Kuandaa kuweka Kumbukumbu na kutoa taarifa za utekelezaji za kila mwezi, robo mwaka na mwaka mzima.
  • Kufuatilia, kutoa taarifa nakupangamikakati ya kuzuiamagonjwayoteyanayozuilika kwa chanjo.
  • KuchukuaSampuli za AFP kwa jamii juu ya magonjwayanayozuilikakwa chanjo.
  • Kusimamianakuratibu siku za chanjo za kitaifa.
  • Kuweka Kumbukumbu ya chanjona vifaa vyotevinavyoingia kutoka katika kitengo.
  • Kuhakikisha kunakuwepo na ushirikishwajikikamilifukwa wadau mbalimbali katika sekta ya Afya na sektanyingineilikuboresha huduma ya chanjo
  • Kupanga na kusimamiautoaji wa huduma ya chanjo katika vijijivilivyombali na vituo vya huduma kwa njia ya mkoba (mobile clinic) 

2.KITENGO CHA DAWA

Kitengo cha dawa kinatoa huduma za;

  • Dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI na kuzuia ya maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto .
  • Dawa na vifaa vya uzazi wa mpango
  • Dawa za kifua kikuu na ukoma
  • Vifaa vya upimaji wa maabara
  • Dawa za Huduma za dharura na majeruhi.
  • Dawa za magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele (Neglected tropical diseases)
  • Dawa za magonjwa ya maambukizi mbalimbali (Essential Medicines).

2. Kitengo cha Kifua Kikuu/Ukoma

Kitengohikihufanyashughulizifuatazo;

  • Kuratibu Shughuli zote za Kifua naUkoma Wilayani.
  • Kusaidiawafanyakaziwenginejinsi ya kutambua wagonjwa wa Kifua Kikuu na wanarudiamatibabu na vipimokupelekwaMaabara kwa uchunguzi zaidi.
  • Kukusanyatakwimu juu ya magonjwana tiba zake pia kutoa taarifa zake na maelekezo ya matumizi ya takwimuhizo kila robo mwaka na mwaka mzima.
  • Kuhakikisha kuwa vipimo vya makohozivya wagonjwa wapyawa Kifua Kikuu na wagonjwa wapya wa kifua kikuu wanaorudiamatatibabuvinapelekwa katika maabara ya juu kwa uchunguzi.
  • Kutekelezamikakatiyoteinayohusianana Kifua Kikuu na Ukoma kwa kusaidiana na wafanyakaziwaliochiniyakeuangalizi wa Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma.
  • Kuwepoushirikianowa wadau wengi katika kuboreshaelimu ya juu ya Kifua Kikuu na Ukoma.
  • Kusimamianakufuatilia kwa karibu wagonjwa waliochini ya matibabu ya Kifua Kikuu na Ukoma na kuweka Kumbukumbu na kutoa taarifa zakekadriinavyohitajika.

 

3. Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto

Kitengo hiki hufanya shughuli zifuatazo;

  • Kusimamia huduma ya akina mama wajawazito (comprehensive ANC) vituonina kliniki ya mkoba.
  • Kutoa huduma ya uzaziwampango katika vituo vya kutolea huduma na kliniki ya mkoba.
  • Ukusanyaji wa taarifa za Mtuha pamoja na kuingiza kwenye mfumo wa DHIS 2
  • Kuendelakuhamasisha jamii umuhimuwakujifungulia katika vituo vya Afya ilikupunguza vifo vya akina Mama na Watoto wachanga.
  • Kusimamiautoajiwadamu (DBS) kwa watotowaliozaliwa na akina mama wenye maambukizi na kutuma KCMC.
  • Usambazajiwa dawa na vifaa tiba RCH kama SD Bioline, syphilis kit, MRDT kit, fefo, SP, mebandazole na kadizote RCH1, RCH4 na RCH5.
  • Kufunyauchunguziwadalili za awali wa shingo ya kizazi.
  • Kuelimisha jamii umuhimuwaakinamajwazitokuwahi kliniki maraanapopojigundua kuwa ni mjamzito.

 

Jengo la upasuaji katika kituo cha afya Orkesumet

 

 

4. Kitengo cha Afya Mazingira

 

Kitengohikihufanyashughulizifuatazo;

 
  • Ukaguzi wa afya na Usafi wa Mazingira Wilayani
  • Ukaguzi wa Maduka ya Vyakula,Dawa na VipodoziWilayani
  • Ufuatiliaji wa mienendo ya magonjwa ya milipuko,kuambukiza na yasiyoyakuambukiza
  • KusimamiaSheria no 1 ya Afya ya Umma(2009),SheriayaAfya na Usalamamahala pa kazi(Occupatinal Health and Safety 2003),Sheria ya Usimamizi wa Chakula,Dawa na Vipodozi 2003),Sheria yausimamizi wa Mazingira 2004 na kanunizake.
  • Uthibiti wa Waduduwaenezaomagojwa ya binadamu.
  • Uendeshaji wa taka ngumu na majitaka  katika maeneo yanayozalisha taka hizo.
  • Kuratibu Shughuli za Afya kinganaUsafi wa Mazingira Wilayani.
  

5. Kitengo cha Maabara

 

Kitengohikihufanyashughulizifuatazo;

 
  • Kufuatilia vitendanishi kwa ajili ya kazi za maabara
  • Kufuatilia uhamasishaji wauchangiaji wa damundani ya Wilaya.
  • Kuwashauriwatendajiwamaabara katika kazi zao.
  • Kufuatiliautendaji kazi za maabaraili kutoa majibu sahihi.
  • Kutoa taarifa za maabarakwauongozi wa juu.
  

6. Kitengo cha Macho

 

Kitengohikihufanyashughulizifuatazo;

 
  • Kufanya upasuajiwa macho ya mtoto wa jicho.
  • Kufanya kliniki ya mkobana kufanya upasuaji wa vikope katika Kata zotendani ya Wilaya.
  • Kufuatilia wagonjwa waliofanyiwaupasuajimdogowa macho pamoja na kutolewanyuzi.
  • Kufanya Usimamizi shirikishi pamoja nakufuatilia wagonjwa.
  

 

 

Daktari akifanya upasuaji wa macho

 

7. Kitengo cha Afya ya kinywanameno

 

Kitengohikihufanyashughulizifuatazo;

 
  • Kufanya kazi za kinga – tiba ya magonjwa ya kinywa
  • KushirikiananaWataalamwengine kwenye jamii kama Walimu na wahudumu wa Afya vijijini kwenye kuboresha afya ya kinywa.
  • Kugunduamatatizoambayosiyo ya kawaidakinywaninakuchukua hatua zinazostahili.
  • Kung’oanakuzibameno.
  • Kutoa huduma ya kwanza matatizoyatokanayo na ajali
 

 

 

8. Kitengo cha iCHF

 

Kitengohikihufanyashughulizifuatazo;

 
  • Kuhamasisha jamii kujiungana Mfuko wa jamii ulioboreshwa.
  • KuwasimamiakwakaribuWaratibu wa Tarafa wa Mfuko wa afya ya Jamii ulioboreshwa.
  • Kuandaa taarifa za kila mwezina robo mwaka wa Mfuko wa afya ya Jamii.
  • Kuhakikisha akaunti za vituo zinafanya kazi.
  • Kuandaa na kuwasilisha maombi ya tele kwa tele kwa Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa.
  • Kuhakikisha taratibuzote za fedha za Mfuko waBima ya afya ulioboreshwazinafuatwa na wakuu wa vituo.
  • Kutoa mrejeshowa Shughuli za iCHF kwa Mganga Mkuu Wilaya.
  • Kutunza Kumbukumbu sahihi za iCHF
 

Uhamasishaji ukifanyika wa wanajamii kujiunga na mfuko wa afya ya jamii ulioboreshwa 

 

9.Kitengo cha BIMA YA AFYA

 

Kitengohikihufanyashughulizifuatazo;

 
  • Kuhakikinakupitishafomumpya za wanachama wa Bima ya Afya.
  • Kutuma maombi fedha za madai za vituo vya kutolea huduma kwenye Ofisi za BimaMkoa
  

10. Kitengo cha Ustawiwa jamii

 

Kitengohikihufanyashughulizifuatazo;

 
  • Kusimamiautekelezajiwasheria, kanuni, miongozo na taratibu mbalimbali za nchi kama vile Sheria ya Mtoto Na. 21 ya Mwaka 2009, Kanuni ya Usalama wa MtotoSura 13 ya Mwaka 2014.
  • Kuendeshamahojiano (Interview) kwa familia zenye matatizo ya kijamii kama vile watotokuzaliwanje ya ndoa, migogoro ya ndoa, Matunzo ya watotowaliotelekezwa na kadhalika.
  • Kushirikiana na taasisi, idara, vitengo, ofisi na vyombo mbalimbali kwa maslahi ya ustawi wa makunditete katika jamii kama vile watoto, vijana, wanawake, wanaume, wazee, watu wenyeulemavu pamoja na watu wenyeshida mbalimbali za kijamii kama vile Jeshi la Polisi, Mahakama, Vituo vya Kutolea Huduma za Afya, Ofisi za MaafisaWatendaji Kata na Vijiji
  • Kutoa elimumashuleni na katika jamii (Preventive Social Work)
  • Kukusanyatakwimu za watu wenyeulemavu, wazee pamoja nawatotowalio katika mazingirahatarishi.
  • Kufanya ukaguziwamazingira (Home visits) zinamoishi familia zenye matatizo na kuandaa taarifa ilikufahamuhalihalisi ya familia ilivyo kwa ajili ya kutoa hoja na mapendekezo ya namna ya kuiwezeshakukabilimaisha.
  • Kutembeleanakukagua vituo vya kuleleawatotowadogomchana na makao ya watotoyatima/wenyeshidailikufahamuubora, viwangovinavyohitajika na elimuwalionayowalezi na wamiliki wa vituo.
  • Kushirikiana na vyama vya watu wenyeulemavu kama vile Chama cha Walemavu wa Viungo Tanzania (CHAWATA), Chama cha Albino Tanzania (CAT), Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA), Chama cha Wasioona Tanzania (TLB), Chama cha Viziwi na Wasioona Tanzania (TASODEB), Chama cha Walemavu wa Afya ya Akili Tanzania (TUSPO), Chama cha wenyeMatatizo ya Ngozi Tanzania (PSORATA) na kadhalikailikubuni na kupangamipango na mikakatiinayoendana na mahitaji yao.
  • Kuendeshauraghbishikwa viongozi, wadau na jamii kwa ujumla juu ya huduma shirikishi jamii (community-based services) kwa wazeewasiojiweza na watu wenyeulemavu.
  • Kupokea, kuchambuanakuandaa orodha ya maombi ya uandikishaji wa vituo vya kuleleawatotowadogomchana (DCC), Malezi ya kambo (foster care), vituo vya malezi ya watotowadogo.
  

11.Kitengo cha Ukimwi

 

Kitengohikihufanyashughulizifuatazo;

 
  • Kuratibu na kuongoza Shughuli zotezinazohusianamagonjwa ya ngono (STI)Ukimwindani ya Wilaya kwa kuwshirikisha jamii na washirikawenginebinafsi na ya Serikali – kuhakikisha sera, miongozomikakatimbinu na sheriazinazohusiana eneo tajwa zinatekelezwaipasavyo.
  • Kuhakikisha takwimuzotezinakusanywandani Ya Wilaya nakujumuishwa pamoja kwa kila mwezi na kutumwa kwa Mganga Mkuu wa Mkoa na Mratibu wa UkimwiMkoaambaonaowatatumaripoti katika fomu maalumu Wizarani (NACP).
  • Kuratibu mafunzo yote juu ya magonjwa ya ngononaUkimwi Wilayani.
  • Kuratibu Shughuli za utoaji huduma kwa wagonjwa waliopohospitalin na wale waliokomajumbani.
  • Kupokea kutunzanakugawanya vifaa au nyenzonyinginezilizotolewawilani kwa ajili ya uthibiti wa magonjwa ya ngono na Ukimwi.
  • Kuandaa taarifa za Shughuli zilizofanyika na fedha zilizotumika
  • Kutunza register ya wagonjwa wa UKIMWI.
   

12.Kitengo cha Huduma kwa wagonjwa majumbaniwanaoishi na maambukizi ya VVU

 

Kitengohikihufanyashughulizifuatazo;

 
  • Kuandaa mipango ya hduma za HUWANYU za Wilaya.
  • Kuhakikisha wateja wote wenye maambukizi wanaingia kwenye kliniki ya matunzo na Tiba na hduma za HUWANYU, CTC, PMTCT, Children  TB
  • Kushirikianana CBHS provider kutembelea wagonjwa majumbani.
  • Kuandaa mikutano ya kila mwezina robo mwaka ya CBHS na Kuandaa mipango ya kazi.
  • Kuhakikisha vitendea kazi vipona dawa kwa wahudumu ngazi ya jamii.
  • Kuandaa ripoti ya mwezi, robo nakuzituma Mkoani na Mdau.
  • Kuhakikisha CBHS provider wanahudhuria kliniki nakusaidiana na Watumishi wa CTC, RCH na kupata wagonjwa wapya.
  • Kuhakikisha jamii inapataelimu ya VVU/UKIMWI katika vikao kupitia CBHS.
  • Kupunguzaunyanyapaandani ya jamii na familia.
  • Kuinuakiwango cha upimaji waVVundani ya familia zilizoathirika na ambazo azijaathirika.
  • Kutafuta wagonjwa walioasi dawa kabala ya kupoteanakuwarudisha katika kliniki za matunzo na Tiba, RCH kwa kushirikiana na DACC,DRCHCO.
  • Kushirikianana CHMT katika Usimamizi Shirikishi kuboresha huduma ngazi ya jamii.
  • Kuhudhuria vikao vya CBHS.
  • Kuundavikundi vya Wanaoishina Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
  

13.Kitengo cha Lishe

 

Kitengohikihufanyashughulizifuatazo;

 
  • Kutoa elimu ya lishe kwa makundi maalumu kama wajawazito, wanaonyonyesha ,wagonjwa wa kisukari.
  • Kufanya tathimini ya hali ya lishe
  • Kuchambuatakwimu mbalimbali za kilishe kwa ajili ya kuzitumiakutekelezamkakati wa kitaifa wa kupunguzautapiamlo
  • Kusimamiashughuli za lishezinazofanywana wadau mbalimbali Wilayani.
  

14. Kitengo cha kifua Kikuu naUkimwi

 

Kitengohikihufanyashughulizifuatazo;

 
  • Kutoa huduma za kifua kikuu  na UKIMWI na kutibu.
  • Kuratibu huduma shirikishi za Kifua Kikuuna UKIMWI Wilayani kamamwongozo wa Taifaunavyoelekeza.
  • KumshaurikitaalumMganga Mkuu wa Wilaya kuhusuhali ya kifua kikuu na UKIMWi Wilayani.
  • Kutoa ushauri wakitaaluma kwa wafanyakazina Taasisizinazotoa huduma za kifua kikuu na UKIMWI.
  • Kusimamiautekelezajiwa huduma hizi katika katika vituo vya afya.
  • Kuratibumikutano ya utekelezajiwa huduma za kifua kikuu na UKIMWI Wilayani.
  • Kutoa taarifa za utekelezaji za robo nanusu mwaka.
  • Kushiriki katika Kuandaa mpangomkakatiwa afya ya Wilayani.
  • Kuhakikisha kuwa vitendea kazi na dawa za kifua kikuu na UKIMWI zipo katika vituo vya afya.
  

15.Kitengo cha Tiba Mbadala

 

Kitengohikihufanyashughulizifuatazo;

 
  • Kuwatambuawagangawa Tiba Asili na Tiba mbadala.
  • Kuwapaelimukuhususheria ya Tiba Asilimbadalana 23 ya mwaka kusajili Shughuli za tiba asili na tiba mbadalaBaraza la Tiba Asili.
  • Kufanya taratibu za usajilikwakugaafomu za maombi ya usajili kwa watendaji wa vijiji/vitongoji.
  • Kutuma fou za maombi ya usajilizilizokamilikakwa Mratibu wa Tiba Asili na tiba mbadala wa Mkoa na hatimayeBaraza la Tiba Asili na Tiba mbadala la Tiafa.
  • Kufuatilialeseni zilizokuwa tayari.
  • Kufanya Shughuli za Usimamizi kwawaganga wa tiba asili na tiba mbadala.
  • Kusimamiasheria ya tiba asili na tiba mbadala na 23 ya mwaka 2002.
   

16.Kitengo cha Magonjwa yasiyopewa kipaumbele

 

Kitengohikihufanyashughulizifuatazo;

 
  • Kuelimisha jamii kuhusumgonjwayalikuwahayapewikipaumbele.
  • Kuhamasisha jamii kuhusuumuhimuwakumeza dawa (tiba kinga) zinazotolewa kila mwaka.
  • Kusimamiana kusambazwa dawa za kingatiba kwenye kila kituo cha tiba ndani ya Wilaya.
  • Kusimamiazoezi la ugawaji dawa za kingatiba kwenye jamii nashuleni.
  • Kuandaa na kutoa taarifa ya zoezi la ugawaji wa dawa za kingatiba kwa kila mwezi.
 

17.KITENGO CHA MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA(NON COMMUNICABLE DISEASES-NCD)

 
  • Kutoa elimu ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama shinikizo la damu,kisukari,saratani nk
  • Kutoa huduma za matibabu
  • Kusimamia program za mazoezi kila mwezi
 

CHANGAMOTO

 

Idara ya afya inakabiliwa na changamoto zifuatazo

 
  • Ukubwa wa eneo linalohudumiwa (km za mraba 20,592)
  • Mfumo dume katika jamii husika
  • Mila na tamaduni
  • Mwamko mdogo wa wakina mama wajawazito kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya
  • Uchakavu wa gari la dharura la wagonjwa
  • Uchache wa magari ya kutolea huduma za afya
  • Uchache wa vituo vya kutolea huduma za afya
  

MIKAKATI YA BAADAE

 

Katika kukabiliana na changamoto hizo idara ya afya katika wilaya ya Simanjiro imedhamiria kufanya yafuatayo:

 
  • Kuendelea kutoa elimu katika jamii
  • Kuhusisha wadau mbalimbali katika kutoa huduma
  • Kuendelea kufanya kazi kama timu moja katika kutoa huduma za afya
  • Kufanya uhamasishaji katika jamii
   

                              Kaimu mganga mkuu wa wilaya na uongozi wa kijiji cha loosoito katika  uhamasishaji kuongeza vituo vya kutolea  huduma za afya.

 

Matangazo

  • RATIBA ZA VIKAO VYA MADIWANI 2020 November 20, 2020
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJI WILAYANI SIMANJIRO

    November 11, 2020
  • Ona vyote

Video

Mkuu wa Mkoa afuta vyeo walimu wakuu 42
video Zaidi

Fika kwa Haraka

  • Matokeo kidato cha nne 2021
  • Mission and Vision
  • Organization Structure
  • Completed Projects

Kiungo Muunganisho

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Idara ya Habari-Maelezo
  • Tovuti kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Simanjiro Bomani street-Orkesumet

    Sanduku la Posta: P.o Box 9596,Orkesumet,Simanjiro,Manyara,Tanzania

    Simu: Tel:027-2552225

    Simu: +255-758350936

    Barua pepe: ded@simanjirodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za siri
    • Kanusho
    • Website Map

copyright@2016 Halmashauri ya Wilaya Simanjiro.Haki zote zimehifadhiwa